Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Kupe wanapamba moto dakika za lala salama, huku Lugumi kule Samia!
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kuwa ni haki kwa Watanzania kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan, kwani ndiye kiongozi wa nchi na amekuwa akishuhudia juhudi zake kubwa za kutafuta fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kadogosa alibainisha kuwa, katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia, amemuona akifanya kazi kwa bidii na hata kumsindikiza kwenye safari mbalimbali zinazolenga kutafuta fedha kwa ajili ya kufanikisha miradi kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).
Kauli hiyo aliitoa leo wakati wa misa maalumu ya kumuombea Rais Samia, ambayo pia iliendana na kumbukumbu ya kifo cha baba yake mzazi, Daudi Kungu Kadogosa. Misa hiyo ilifanyika katika mtaa wa Mwakibuga, mjini Bariadi, nyumbani kwa mkurugenzi huyo wa TRC.
“Mimi ni mteule wa Rais Samia. Mara nyingi ninazungumza naye, nakaa naye, na wakati mwingine ninasafiri naye. Namshuhudia mama yetu anavyohangaika kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kwa hiyo, ni haki kabisa kumuombea Rais wetu,” alisema Kadogosa.
Aidha, alitoa wito kuwa Tanzania ina Rais mmoja tu ambaye anapaswa kulindwa na kuombewa na kila Mtanzania ili kufanikisha maendeleo ya taifa.