Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Na hicho ndicho wenzenu wanakitaka ili mpande mabasi yao, ndio maana hujuma zimeanza kwenye kuchelewesha mradi,wanahujumu kwenye kuweka nauli kubwa , na sasa watahujumu kwenye kuchelewesha muda ili ionekane halina tofauti kubwa na basi na baada ya hapo watahujumu miundombinu yake na kazi ya treni ya umeme itaishia hapo tutaendelea kupanda mabasi yao

Hakuna kitu kibaya kama kuruhusu wafanya biashara kuwa viongozi na wenye maamuzi ndani nchi
Kweli,kama walikuwa wanafungulia maji ya bwawa la Mtera kwenda mashambani ili tukose umeme unadhani watashindwa kuhujumu huu mradi!
 
Suala la kula umeme au kutokula hatulijui.

Kama ni 336000/= basi nauli itakua chini sana, tufanye hivi kila kichwa 20000×500=10,000,000/= kurudi dar 20000×500=10,000,000/=

Hapo ukitoa posho na vigharama vidogo, unapata faida sio chini ya m5 to 7 per day. Na kama wakiweza kwenda root 4 kwa siku aise watapiga hela kubwa sana
 
Ndio maana magufuli alisema lazima umeme ushuke bei kwa sababu ikiwa sehemu kubwa unazalishwa kwa maji basi gharama ya uzalishaji lazima itapungua. Uzalishaji kwa njia ya mabwawa ya maji ndio umeme rahisi kabisa. Sasa kina makamba na maharage wake waliona hapo wao wapige kwa kufaidi kwa mishahara na kila aina ya marupurupu manono na upigaji kwa kila namna. Yaani wale wenyewe upungufu mkubwa kwenye gharama ya uzalishaji wa umeme. Wananchi tusikubali ubadhirifu tanesco au serikalini kote. Mitambo itakapokua yote inafanya kazi ni lazima wosia wa magufuli utekelezwe. Tena sio kupunguza bei kwa visenti. Umeme lazima ushuke hadi wazalishaji wa viwandani na watoa huduma waone ulazima kupunguza bei ya bidhaa zao.
Aah wapi! Tanzania hii? Sahau kabisa..tuliambiwa hivi hivi wakati gesi ya Mtwara inafanyiwa utafiti. Imepatikana ila bado bei ya umeme inapanda.
 
Basi nauli inaweza kuwa 500-600 humo. Ikizidi hapo.
Eenh Mwenyezi Mungu nisaidia na mimi niwe kati ya wahusika katika uongozi wa nchi hii siku za. Usoni. Serikali inapiga hela safi sana.
Ndugu yangu kwa nauli walizowahi kutangaza/kupendekeza watu saba tu wanalipia umeme wa train hiyo na change inarudishwa! Abiria wengine wote waliobaki watakuwa wanalipia gharama za miundo mbinu!! Upo hapo!!??
 
Ndugu yangu kwa nauli walizowahi kutangaza/kupendekeza watu saba tu wanalipia umeme wa train hiyo na change inarudishwa! Abiria wengine wote waliobaki watakuwa wanalipia gharama za miundo mbinu!! Upo hapo!!??
Nipo acha nitafute nafasi serikalini
 
Back
Top Bottom