Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kwa umeme huo waliotumia nitashangaa kama nauli ya dar moro kama itazidi sh 3000
Swala la gharama lina chukua mpaka fedha ya mikopo na gharama za ujenzi na ukarabati na muda wa kulipa mikopo ila zinatakiwa kuwa chini kidogo tofauti na mabasi .
 
Wamechukua muda sababu....hawawezi enda full speed...kwenye test....mdogo mdogo test ya pili wataongeza speed kidogo.....test 3 etc....then wataweka constant speed wakianza safari biashara
Hao wanao taka speed hovyo hovyo ni sawa na wapumbavu wanaodhani mtu akinunua gari lenye speed ya km250 kwa saa basi ni lazima hatumie hiyo speed tena muda wote aendeshapo hiyo gari
 
chama cha kupinga watapinga
Hata facts ni kupinga.

Walitakiwa watueleze sababu ya treni ya 180 km/h inakwenda speed ya 38 km/h.

Kama hayo ndiyo majaribio yenyewe... Si waseme tu kwamba tunaanza 30, then 70, then 120 mpaka wafike hiyo speed waliyotuambia mwanzo.
 
mwisho tutasikia imetumia umeme wa 560, ila watuambie limetumia unit ngapi? ama watuambie hizo pesa ni sawa na unit ngapi za umeme?. kichwa kilikuwa kinavuta behewa ngapi toka dar hadi moro?, kimetembea speed ngapi?, na unit za umeme kimetumia ngapi?, watuambie na unit moja ya umeme wa sgr ni kiasi gani?...tuone uhalisia upo wapi
Na tunajua mzigo ukiongezeka na nguvukazi pia hivyo siku ikiwa full watu na mizigo itatumia umeme wa sh ngapi??

Maswali ya kujiuliza ni mengi, ila mi nafikiri tubaki tu kwenye suala la mwendokasi ambalo ndilo la msingi zaidi, kuwahisha ufikaji ulio salama na wa haraka katika maeneo ya mbali kama Mwanza n.k
 
Kwa hiyo lengo la kufanya test ni kutaka kujua hiyo train inatumia umeme wa sh. ngapi au mimi ndio sijaelewa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) imetumia umeme wa Sh336,000 katika safari ya abiria ya majaribio kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Morogoro na kurudi leo Februari 26, 2024.

“Miundombinu ya treni ya umeme ni gharama kubwa ukilinganisha na ile ya inayotumia mafuta lakini kwenye gharama za uendeshaji wa treni ya mafuta ni mara tatu ukilinganisha na treni ya umeme,” amesema Kadogosa alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM.

Akizungumzia kuhusu nauli za abiria zitakazotumika, Kadogosa amesema shirika hilo limewasilisha mapendekezo yake kwa Latra yenye jukumu la kutangaza nauli hizo.

Ameongeza kuwa, upatikaaji wa mizigo mingi utachangia kupungua kwa nauli kwenye treni ya abiria na kufanya watu wengi wawe na uwezo wa kumudu bei za kupanda treni hiyo.

“Tunatarajia kupata fedha zaidi kwenye mizigo na ndio maana unaona tunajenga reli kwenda Msongati sababu kuna machimbo ya Nikel, tunakwenda kwa sababu tutapata mzigo kutoa kule na kupeleka bandarini. Upatikanaji wa mzigo ndio utatufanya tusiwe na bei kwenye treni ya abiria,” amesema.

Treni ya umeme ya abiria imefanya safari ya kwanza ya majaribio hii kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro huku ikitumia takribani saa nne kwenda na kurudi.
Ndio maana magufuli alisema lazima umeme ushuke bei kwa sababu ikiwa sehemu kubwa unazalishwa kwa maji basi gharama ya uzalishaji lazima itapungua. Uzalishaji kwa njia ya mabwawa ya maji ndio umeme rahisi kabisa. Sasa kina makamba na maharage wake waliona hapo wao wapige kwa kufaidi kwa mishahara na kila aina ya marupurupu manono na upigaji kwa kila namna. Yaani wale wenyewe upungufu mkubwa kwenye gharama ya uzalishaji wa umeme. Wananchi tusikubali ubadhirifu tanesco au serikalini kote. Mitambo itakapokua yote inafanya kazi ni lazima wosia wa magufuli utekelezwe. Tena sio kupunguza bei kwa visenti. Umeme lazima ushuke hadi wazalishaji wa viwandani na watoa huduma waone ulazima kupunguza bei ya bidhaa zao.
 
Umeme hauwezi kushuka bei, kuna makampuni yanayoiuzia umeme TANESCO yana mikataba mpaka ya miaka 20 mbele yanalipwa capacity charge. Tena mamilioni kwa siku awe amewasha mtambo au hajawasha yeye analipwa, akiwasha kuwauzia umeme ndio balaa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) imetumia umeme wa Sh336,000 katika safari ya abiria ya majaribio kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Morogoro na kurudi leo Februari 26, 2024.

“Miundombinu ya treni ya umeme ni gharama kubwa ukilinganisha na ile ya inayotumia mafuta lakini kwenye gharama za uendeshaji wa treni ya mafuta ni mara tatu ukilinganisha na treni ya umeme,” amesema Kadogosa alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM.

Akizungumzia kuhusu nauli za abiria zitakazotumika, Kadogosa amesema shirika hilo limewasilisha mapendekezo yake kwa Latra yenye jukumu la kutangaza nauli hizo.

Ameongeza kuwa, upatikaaji wa mizigo mingi utachangia kupungua kwa nauli kwenye treni ya abiria na kufanya watu wengi wawe na uwezo wa kumudu bei za kupanda treni hiyo.

“Tunatarajia kupata fedha zaidi kwenye mizigo na ndio maana unaona tunajenga reli kwenda Msongati sababu kuna machimbo ya Nikel, tunakwenda kwa sababu tutapata mzigo kutoa kule na kupeleka bandarini. Upatikanaji wa mzigo ndio utatufanya tusiwe na bei kwenye treni ya abiria,” amesema.

Treni ya umeme ya abiria imefanya safari ya kwanza ya majaribio hii kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro huku ikitumia takribani saa nne kwenda na kurudi.
Kuna watu wahujumu usafiri wa SGR ili kulinda wenye mabasi , wakati usafiri wa treni ndio mzuri , sababu ya muda unaotumia njiani na pia nafasi ya kusoma, kutembea, na kutumia maliwato bila kusumbua abiria wengine.
 
Kuna wale wauza dawa za minyoo na sumu ya panya wasiruhusiwe ndani ya tren pia kuingia na mifugo kama kuku n.k
Mkuu jana tu nimeshuhudia kituko cha mwaka, mwandishi aliyealikwa kwenye majaribio ya treni ya mwendokasi alionekana akisifia finishing ya jengo la abiria kwa kushika ukuta na kuchora kwa vidole vyake, alionekana kutest milango kwa kuigongagona na mbaya zaidi alionekana akikwangua na kucha vile viti,hata kuuma viti kwa meno!.....
Fikiria baada ya mwaka mmoja haya mabehewa na jengo la abiria vitakuwa na hali gani baada ya miaka miwili? 😲
 
mwisho tutasikia imetumia umeme wa 560, ila watuambie limetumia unit ngapi? ama watuambie hizo pesa ni sawa na unit ngapi za umeme?. kichwa kilikuwa kinavuta behewa ngapi toka dar hadi moro?, kimetembea speed ngapi?, na unit za umeme kimetumia ngapi?, watuambie na unit moja ya umeme wa sgr ni kiasi gani?...tuone uhalisia upo wapi
Na vichwa walivyo nunua gharama zake za uendeshaji zipoje, isije kuwa bei ya kununua rahisi lakini gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo tunapigwa kote kote.
 
Umeme wa laki 3+, sawa sio kesi, kwa idadi ya abiria inayobeba treni, behewa moja kule kajamba nani ni kama watu 60 hivi(sina hakika ni makadirio) hawa wana bei zake, bado 2nd class, bado 1st class kila daraja na nauli yake, still si shida kabisa, watwambie tren ya mafuta ilikuwa inatumia diesel kiasi gani mpaka moro ili tuweze linganisha.
diesel itakuwa nyingi sana bro. na moro inaweza tumia masaa 10
 
Back
Top Bottom