Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) imetumia umeme wa Sh336,000 katika safari ya abiria ya majaribio kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Morogoro na kurudi leo Februari 26, 2024.

“Miundombinu ya treni ya umeme ni gharama kubwa ukilinganisha na ile ya inayotumia mafuta lakini kwenye gharama za uendeshaji wa treni ya mafuta ni mara tatu ukilinganisha na treni ya umeme,” amesema Kadogosa alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM.

Akizungumzia kuhusu nauli za abiria zitakazotumika, Kadogosa amesema shirika hilo limewasilisha mapendekezo yake kwa Latra yenye jukumu la kutangaza nauli hizo.

Ameongeza kuwa, upatikaaji wa mizigo mingi utachangia kupungua kwa nauli kwenye treni ya abiria na kufanya watu wengi wawe na uwezo wa kumudu bei za kupanda treni hiyo.

“Tunatarajia kupata fedha zaidi kwenye mizigo na ndio maana unaona tunajenga reli kwenda Msongati sababu kuna machimbo ya Nikel, tunakwenda kwa sababu tutapata mzigo kutoa kule na kupeleka bandarini. Upatikanaji wa mzigo ndio utatufanya tusiwe na bei kwenye treni ya abiria,” amesema.

Treni ya umeme ya abiria imefanya safari ya kwanza ya majaribio hii kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro huku ikitumia takribani saa nne kwenda na kurudi.
chama cha kupinga watapinga
 
Msongati ni wapi?
 
Na hicho ndicho wenzenu wanakitaka ili mpande mabasi yao, ndio maana hujuma zimeanza kwenye kuchelewesha mradi,wanahujumu kwenye kuweka nauli kubwa , na sasa watahujumu kwenye kuchelewesha muda ili ionekane halina tofauti kubwa na basi na baada ya hapo watahujumu miundombinu yake na kazi ya treni ya umeme itaishia hapo tutaendelea kupanda mabasi yao

Hakuna kitu kibaya kama kuruhusu wafanya biashara kuwa viongozi na wenye maamuzi ndani nchi
Tunakosa tu viongozi wenye maono na nia dhabiti.

Wengi ni wapigaji tu na wabinafsi.
 
Atuwekee hapa mita iliyosoma hayo matumizi ya umeme, vinginevyo itakuwa chai kama chai nyingine tu...
 
Kitumie kichwa chako kufikiri.

Kati ya Dar mpaka Moro kuna vituo zaidi ya 10, na vituo vyote treni inasimama. Itatumia vipi hizo dk 30?!
Hii ni for business only DK 3 inatosha kushusha na kupakia kwa Ivyo Vituo. Ukiweka hapo ni DK 30 kushusha na kupakia zinatosha Sana.
 
Kashusha gharama za umeme uliotumika, labda usiwe na uelewa na issue za motor ndio utakubali huo ujinga anaousema.
Maajabu huwa hayaishi huko kila mmoja na lake
Gharama zitakuja nyingi sana za matengenezo na uendeshaji wa shirika na yeye anawaza nauli na umeme unatumika mdogo na nauli zitashuka what a joke

UK dereva wa Train anakula mshahara wa tsh 15 million kwa mwezi na bado wanaandamana ingawa ni mkubwa sana kwa dereva

Yote hiyo kwa nauli wanazotoza ni kubwa sana means wanapata faida kubwa
Hebu tusubiri tuone
 
Kashusha gharama za umeme uliotumika, labda usiwe na uelewa na issue za motor ndio utakubali huo ujinga anaousema.
Ungejua mimi ninafanya issue gani usingesema kitu hicho nimekuambia treni lina mita kama za kenye gari tumia akili kama vipi google ujue treni zinatumia unit ngapi kwa 1km....mlio mpinga jpm mnaanza kuwewe seka baada ya kuona akilikubwa ya mzalendo kiuchumi hii ndiyo sababu nchi jirani zinazo zunguka tz kuachana na reli ya kenya na kuangalia kijiunga na ya tz hadi mchina wa kenya alivunjika moyo kwa sababu ya vision ya jpm siyo huyu kahaba anaye nunua saa 4 kila moja kanunua mil 200 na shanga za kiunoni za mil67 na vikuku na vupi vya halili vya sh mil 1 kila kimoja kana kwama hakivaa hivyo vitu hatokufa na kuoza kaburini ..... ukisikia msemo wa mazaa faka ndiyo huyu sasa ....stupid muisiharamu
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) imetumia umeme wa Sh336,000 katika safari ya abiria ya majaribio kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Morogoro na kurudi leo Februari 26, 2024.

“Miundombinu ya treni ya umeme ni gharama kubwa ukilinganisha na ile ya inayotumia mafuta lakini kwenye gharama za uendeshaji wa treni ya mafuta ni mara tatu ukilinganisha na treni ya umeme,” amesema Kadogosa alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM.

Akizungumzia kuhusu nauli za abiria zitakazotumika, Kadogosa amesema shirika hilo limewasilisha mapendekezo yake kwa Latra yenye jukumu la kutangaza nauli hizo.

Ameongeza kuwa, upatikaaji wa mizigo mingi utachangia kupungua kwa nauli kwenye treni ya abiria na kufanya watu wengi wawe na uwezo wa kumudu bei za kupanda treni hiyo.

“Tunatarajia kupata fedha zaidi kwenye mizigo na ndio maana unaona tunajenga reli kwenda Msongati sababu kuna machimbo ya Nikel, tunakwenda kwa sababu tutapata mzigo kutoa kule na kupeleka bandarini. Upatikanaji wa mzigo ndio utatufanya tusiwe na bei kwenye treni ya abiria,” amesema.

Treni ya umeme ya abiria imefanya safari ya kwanza ya majaribio hii kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro huku ikitumia takribani saa nne kwenda na kurudi.
Hii biashara ni kichaa kuanzia mwanzo. Hela zilizochozewa kwenye huu upuuzi, zingetumika kujenga barabara za lami nchi nzima; tungepiga hatua kubwa sana kama Taifa.
 
Back
Top Bottom