Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Ulipotelea wapi?
Kama mkurugenzi anasema gharama ya nishati ni ndogo na lengo ni kupata pesa kupitia kubeba mizigo, kwanini usafiri huo kwa abiria usiwe bure kabisa au ukawa sawa na bure kabisa (labda buku) ili watanzania wengi wafaidi matunda ya kodi zao?
 
"kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro huku ikitumia takribani saa nne kwenda na kurudi"! Mbona sawa na kupanda basi la Shabibby.
Ndio Treni yenu ya Speed feki Kutoka mjini Dar kwenda Morogoro na kutoka Morogoro kwenda Dar masaa 4 Duhhh kazi kweli ipo Si bora upande basi kuliko kupanda hiyo Treni?
 
Hapo halikuwa na abiria kivile limekula umeme Ivo sasa ngoja liongeze mabehewa libebe na abiria uone umeme wake utakuwaje, bado linakula umeme Ilo kwa kuliangalia tu Kwanza lizito.
Weka calculation ya energy consumption per km with all assumptions acha siasa
 
Kama ni hivyo, nauli Dar - Moro iwe tsh5000 na Mabus yabaki kuwa utalii tu Kwa watu ambao hawana haraka.

Tukiwa na akili hii train inaweza kuwa game changer kwenye mambo mengi sana.
Mabus mengi ya kwenda kanda ya ziwa yanaweza kuanzia Morogoro, wakazi WA Morogoro wanaweza kufanya kazi Dar, wakazi wa Dar wanaweza kufanya kazi na biashara Moro.
Mminyano unaweza kupungua Dar es salaam, ajali kati ya Dar - Moro -dom zinaweza kupungua au kuondoka kabisa.

Serikali iharakishe ujenzi wa reli ifike Dodoma na Mwanza haraka ili kuondoa ajali barabarani na kuongeza speed ya ukuaji uchumi, maana Dar to Bukoba kupita pale Busisi darajani safari inaweza kuwa fupi mtu akishuka Mwanza na train then Bukoba inafikika kirahisi the Burundi na Rwanda.

Mwisho, Mwenyezi Mungu amrehemu JPM na kumfanyia wepesi kwenye safari yake kwa kujitoa kwake na maono yake dhidi ya nchi hii.
 
Sawa .....

Ila we mkurugenzi punguza domo domo maneno mengi fanya kazi
Watu wataona matokeo tu

Ova
 
"Kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro huku ikitumia takribani saa nne kwenda na kurudi"! Mbona sawa na kupanda basi la Shabibby.
Na hicho ndicho wenzenu wanakitaka ili mpande mabasi yao, ndio maana hujuma zimeanza kwenye kuchelewesha mradi,wanahujumu kwenye kuweka nauli kubwa , na sasa watahujumu kwenye kuchelewesha muda ili ionekane halina tofauti kubwa na basi na baada ya hapo watahujumu miundombinu yake na kazi ya treni ya umeme itaishia hapo tutaendelea kupanda mabasi yao

Hakuna kitu kibaya kama kuruhusu wafanya biashara kuwa viongozi na wenye maamuzi ndani nchi
 
mwisho tutasikia imetumia umeme wa 560, ila watuambie limetumia unit ngapi? ama watuambie hizo pesa ni sawa na unit ngapi za umeme?. kichwa kilikuwa kinavuta behewa ngapi toka dar hadi moro?, kimetembea speed ngapi?, na unit za umeme kimetumia ngapi?, watuambie na unit moja ya umeme wa sgr ni kiasi gani?...tuone uhalisia upo wapi
Tusingeweza kutoa maelezo hayo kutoka na hadhira.hayo mengine ataelezwa CAG kwa niaba yako na wengine, wewe tosheka na ulichoambiwa kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom