Kadri umri unavosogea napoteza uwezo wa kusikia kinachoendelea around napokuwa usingizini

Kadri umri unavosogea napoteza uwezo wa kusikia kinachoendelea around napokuwa usingizini

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
WAKUU nachukia na nashindwa kukubaliana na UKWELI na hali halisi.

Nilijigundua nina uwezo flani tangu nilipokuwa o level.

Kifupi ni kwamba ninauwezo wa kuskia kinachoendelea napokuwa nimelala/kusinzia.

Uwezo huu ulikuwa mkubwa kipindi nipo chuo yani kuna siku washkaji hawakuanini nilikuwa nimelala kwa takribani masaa ma2-2.5.

Nilipoamka washkaji wakaanza kunacharazia we jamaa unalala mchana imekuwa mjamzito?

Huwa sipendi watu naoishi nao wajue kwamba nina huu uwezo kwasababu nahisi ni kitu ambayo inaweza kuwafanya wakaishi namimi kwa machare na wasiwasi.

Ila jamaa aliporopoka vile nikajikuta namm naropoka "we unadhani nalalaga kizembe mloongea naweza kuwambia" nikaanza kuwambia baadhi ya mambo wakaanza kusema haukuwa umelala nikawambia mimi nilikuwa nimelala.

Kwanzia siku hiyo jamaa walikuwa makini sana kuongea ongea mambo Yao napokuwa rum nimelala.

Yani mimi nikiwa nimelala naweza kuskia na kukumbuka nikiamka yale yote niloskia nilipokuwa usingizini.

Na pia ukinigongea au kuniamsha kabla hata hujaniita jina nishastuka kwahyo huwa nawaachaga waniite tu kwa ushahidi na huwa wananiita mara moja tu nakuwa hewani.

Hata alarm huwa siwekag yani kama nahitaj kuamka asubuhi mapema bas about dk20 kabla nakuwa nishaamka tayari.

Sasa naona KADRI UMRI UNAVOSOGEA napungukiwa na huu uwezo.

Wataalamu vipi nitumie vyakula au dawa gani ili nibakie na uwezo wangu?
 
100% tupo sawa na umri unavyosogea napata experience sawa sawa na wewe.....
Pia naweza kujicontrol nini nifanye napokua ndotoni na kuikumbuka ndoto yote japo naota ndoto mara chache nowadays.
 
Ni vitu tu vinapita nami nilikuwa na uwezo wa kufanya mtihani ndotoni kabla ya asubuhi sijaingia kwenye mtihani nitakapo ishia Hilo swali ndotoni ndio kesho yake asubuhi nitaishia hapo , Pia nilikuwa nikitaka kuanza kuota ndoto labda nahisi kuna watu wanataka kuni chukua automatic naanza kushinda nao kwa maombi mpaka nawashinda nguvu , alafu nashtuka nakuwa katika hali ya kuchoka . Vivyo hivyo darasani nilikuwa sio msomaji hata chuo pia ikitokea nimeshikwa Sup naoteshwa itafanyika maksi itaongezwa upite hata kabla hatujafungua chuo nakuta matokeo yamerekebishwa
 
Duh ni maajabu
 
Nakumbuka pia nilipewa ya kalama ya kuota ukweli....yaani nikiota ndoto basi litatokea jambo iwe kwangu au kwa wanaonizunguka ....nilipopigwa machine tu ikawa ndo basi tena...sahivi ndoto ya ukweli niotayo ni kukojoa kichakani kumbe nakojoa kwa bed 🙄
 
Back
Top Bottom