Aliolewa miaka miwili iliyopita(2017),miezi miwili baada ya kuolewa mumewe akahukumiwa miaka 40 kwa makosa la unyang'anyi wa kutumia nguvu na makosa mengine(alimuoa akiwa nje kwa dhamana)
Bibie akawa amekata tamaa kabisa japokuwa walikata rufaa na kesi ilikuwa inaendelea,akaanza mahusiano ya kimapenzi na jamaaa mmoja kwa siri sana,hivi ninavyoandika uzi huu bibie keshatundikwa mimba na anatarajia mwezi wa nne mwakani ampokee Kijacho.
Wakati anatarajia kupokea huo ugeni mumewe naye kashinda kesi ya unyang'anyi wa kutumia nguvu na kesi zingine kwahiyo atatumikia jela miaka mitatu tu jela,panapo majaaliwa mwezi wa Saba mwakani jamaa atakuwa uraiani,ngoma nzito.B
ibie anawaza kuichomoa mimba ili ainusuru ndoa yake pia maisha yake,maana mumewe sio mtu wa mchezomchezo,kamshirikisha mtu wake kile anachofikiria kukifanya mtu wake anamwambia ukitoa mimba ama zako ama zangu la sivyo ukishajifungua mtoto siku hiyo hiyo niachie nitampeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima ili akija mumeo muendelee na maisha yenu.
Ila sikubali mimba ichomolewe ikichomolewa na chomoka hukohuko,yupo njia panda anawaza hajui afanye nini kote kwa moto,kaniomba ushauri nimeshindwa kumpa ushauri hatimaye nimekuja kwenu wanajukwaa tiririkeni.