Ngwanakilala
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 774
- 1,464
HATIMAYE kitendawili cha nani atakuwa mwandani wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kabwe kimeteguliwa kufuatia mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kuutangazia umma juu ya jambo hilo.
Kafulila alitumbua jipu hilo wakati akitoa utambulisho wa wageni waliofika kwenye tafrija ya harusi yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annex mji Mdogo wa Uvinza wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.
Katika utambulisho huo Kafulila alimtambulisha Anna kuwa ni mchumba wa Zitto na muda si mrefu mambo yatakuwa hadharani.
Kafulila alisema kuwa licha ya kuwa mchumba wa ZITTO pia ni mtumishi wa Ubalozi wa Ireland hapa nchini.
Harusi hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge David Silinde na Deo Filikunjombe na mkewe (wapambe wa maharusi) na Dk. Kitila Mkumbo.
Utambulisho huo wa mchumba wa Zitto unavunja ukimya wa Mbunge huyo kuwa na mahusiano na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mkoa wa Kigoma, Muhonga Ruhwanya na Mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi (Diva The Boss).
Source: Wavuti