The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), David Kafulila, ameungana na wanawake katika kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa ripoti tatu muhimu zinazobainisha mchango wa wanawake katika uchumi na nafasi za uongozi.
Akianza na ripoti ya Taasisi ya UNAC, Kafulila amesema tafiti zinaonesha kuwa asilimia 90 ya kipato cha mwanamke hutumika kwa matumizi ya familia, ikilinganishwa na asilimia 35 ya kipato cha mwanaume nchini Marekani. Akihoji iwapo hali ni sawa kwa Tanzania, amesisitiza umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.
Akitumia Ripoti ya McKinsey, Kafulila amebainisha kuwa iwapo kungekuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi duniani, uchumi wa dunia ungeweza kuongezeka kwa dola trilioni 28.
Katika kuhitimisha salamu zake kwa Siku ya Wanawake, Kafulila ameainisha takwimu kutoka Women Count Report 2020, inayoonesha kuwa kati ya kampuni kubwa 350 katika soko la mitaji la London, ni kampuni 14 pekee zinazoongozwa na wanawake. Hata hivyo, tafiti zinaonyesha kuwa kampuni ambazo walau theluthi moja ya viongozi wake wa juu ni wanawake, hupata faida mara 10 zaidi ya zile zinazowapa wanawake nafasi ndogo za uongozi.
Kafulila amesisitiza kuwa ripoti hizo zinathibitisha kuwa usawa wa kijinsia katika uongozi na uchumi si tu suala la haki, bali pia ni chachu ya maendeleo na ustawi wa jamii na dunia kwa ujumla.
Chanzo: Nipashe