Mr Beast
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 311
- 435
Mhe David Kafulila Mkurugenzi Mkuu wa Ubia nchi PPP amewatoa hofu na mashaka Watanzania kwani Serikali yao ya awamu sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ina nia na dhamira njema dhidi yao.
Kafulila akihojiwa Katika kipindi Cha Television amesema si kosa nchi kukopa kwaajili ya miradi ya maendeleo ila ni dhambi kukopa ili kugharamia mambo kama mishahara na mambo mengine yasiyo ya kimaendeleo yaani matumizi ya kawaida.
Kafulila ameenda mbali zaidi na kuwakumbusha namna Ulaya ilivyojengwa kwa misaada na mikopo toka Marekani ( Marshall Plan ) baada ya Vita kuu ya Pili ya Dunia miaka ya 1948.
Hata hivyo Mhe David Kafulila ameonesha si kweli kwamba Uchumi wa Tanzania unajengwa kwa Mikopo pekee ila ni Kwa sehemu tu,
Kafulila anasema, Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu imekopa fedha nje kiasi cha US$ 5 bilioni wakati Uchumi wake katika kipindi hicho umekua kwa kiasi cha US$ 20 bilioni sawa na tofauti chanya ya US$ 15 bilioni.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa UBia amemsifu zaidi Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyoipokea nchi na kwa kasi hii ya Uchumi ambayo hakuna nchi yoyote Africa Mashariki na Kati kwa miaka hii mitatu iliyofikia kiasi na kasi Kwa kiwango hiki kilichofikiwa na Tanzania ya Dkt Samia Suluhu.
=====