Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
YAJAYO YANAFURAHISHA SANA
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila ameandika haya katika ukurasa wake wa X zamani tweeter,
Kafulila akiifafanua Dira ya Maendeleo ya Taifa la Tanzània ya 2025- 2050 amesema yafuatayo,
1. Kafulila amewataka Watanzania wafahamu kuwa chini ya CCM hii na ifikapo mwaka 2050 Uchumi wa nchi yao utakua kwa Kasi na kufikia $700bn sawa na TZS 1,750 Trilioni.
2. Kafulila amewataka pia Watanzania watambue kuwa chini ya CCM hii Pato lao la mwaka litakuwa na kufikia kati ya $4,500 na $8,000 kwa mwaka yaani hapa karibu kila mtu itakuwa ni kula bata tu Cha msingi tuombe Uzima tu.
3. Kafulila amewataka Watanzania wafahamu yakuwa chini ya CCM hii vipato vyao na Pato la Taifa lao vitaongezeka kwa karibu mara tisa (9) zaidi hii hakuna nchi yoyote itaweza ila Tanzània na Watanzania.
4. Kafulila amewataka pia Watanzania wafahamu kuwa Uchumi wao kwa Sasa ni $80bn lakini chini ya CCM hii na kwa Miaka 25 ijayo utaongezeka kwa Kasi karibu mara 9 zaidi na kufikia 700bn na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi Tajiri zaidi Africa na hii ni chini ya CCM.
5. Kila Mtanzania na afahamu ukuaji huu mkubwa wa maajabu wa Uchumi wa Tanzania na wa mtu mmoja mmoja ni chini ya CCM tu na wala sio vinginevyo.