Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
===
Akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds Media Group Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPP -Centre David Zacharia Kafulila alikuwa na haya ya kusema ;-
"Tafiti zilizofanyika zilionesha kwamba mwaka 2015 mahitaji ya miundombinu yaliyokuwepo yalijitosheleza kwa asilimia 30% tu ya mahitaji ya miundombinu itakayohitajika mwaka 2050 yaani miaka 35 baadae,
Ukitazama mwenendo wa uchumi wa Tanzània wa sasa utagundua kwamba Tanzania itahitaji kujenga uchumi mkubwa zaidi ya ule wa Afrika kusini ya leo ndani ya miaka 25 ijayo.
Kujenga Uchumi zaidi ya Africa ya Kusini ya leo ni jambo ambalo kama tukitumia Kodi na Mikopo pekee hatutaweza kulifikia na hii ndio sababu muhimu ya kutumia PPP ili kufikia matarajio na matamanio haya makubwa ya Watanzania ifikapo mwaka 2050.
David Kafulila anaendelea kwa kusema, " Tunachakata kupata mwekezaji serious wa kujenga barabara ya kisasa ya kulipia kutoka Kibaha- Chalinze mpaka Morogoro.
Jambo la uhakika ni kuwa wawekezaji wanajua pamoja na uwepo wa Reli na treni mpya za SGR bado mahitaji ya usafiri na usafirishaji yataendelea kuwa ni makubwa kila wakati kutokana na ukubwa wa uchumi wa Tanzània unaojengwa chini ya Rais Samia na Chama chake Cha Mapinduzi CCM.
=====