Mwanga wa Jua
Senior Member
- Mar 7, 2025
- 106
- 54
Utafiti hupingwa kwa utafiti🙏===
Akihojiwa na kituo Cha runinga Cha Clouds Media Group Mkurugenzi Mtendaji wa PPP -Centre Bw David Zacharia Kafulila alikuwa na haya ya kusema "Tafiti zilionesha mwaka 2015 mahitaji ya miundombinu yaliyokuwepo yalijitosheleza kwa asilimia 30% tu ya mahitaji ya mwaka 2050.
Ukitazama mwenendo wa uchumi unaona kwamba Tanzania itahitaji kujenga uchumi mkubwa zaidi ya Afrika kusini ya leo ndani ya miaka 25 ijayo jambo ambalo ukitumia Kodi na Mikopo pekee hutaweza na hii ndio sababu muhimu wa kutumia PPP kufikia matarajio na matamanio haya makubwa mwaka 2050.
Tunachakata kupata mwekezaji kujenga barabara ya kisasa ya kulipia Kibaha - Chalinze mpaka Morogoro, wawekezaji wanajua pamoja na uwepo wa SGR ya kisasa bado mahitaji ya usafiri yataendelea kuwa makubwa kutokana na ukubwa wa uchumi unaojengwa na Tanzània chini ya Chama Cha Mapinduzi CCM-alisema Kafulila.
=====
View attachment 3074274