Huyu ni yeye tunayemtarajia?===
Akihojiwa na kituo Cha runinga Cha Clouds Media Group Mkurugenzi wa PPP -Centre Bw David Kafulila alikuwa na haya ya kusema "Tafiti zilionesha mwaka 2015 mahitaji ya miundombinu yaliyokuwepo mwaka 2015 yalijitosheleza kwa asilimia 30% tu ya mahitaji ya mwaka 2050.
Ukitazama mwenendo wa uchumi unaona kwamba Tanzania itahitaji kujenga uchumi mkubwa zaidi ya Afrika kusini ya leo ndani ya miaka 25. Hii inaokuonesha umuhimu wa kutumia PPP kufikia matarajio makubwa.
Tunachakata kupata mwekezaji kujenga barabara ya kisasa ya kulipia Kibaha - Chalinze mpaka Morogoro, wawekezaji wanajua pamoja na uwepo wa SGR ya kisasa bado mahitaji ya usafiri yataendelea kuwa makubwa kutokana na ukubwa wa uchumi unaojengwa "
===
View attachment 3074274