Aliporejea kutoka India alisema mengi, lakini hili la Adan akitaka apewe TANESCO kama mwekezaji nasikia harufu kwasababu wenzetu wamesikia harufu toka kwa Adan.
Namtaka Kafulila aje atwambie hii harufu ya Adan kule India hakuisikia kama siyo kupakazwa na yeye? Ile TICS kachukua Adan. Kafulila kala matapishi yake kupitia sahani ya Adan?
Hili halifai kupingwa hata kidogo ingefaa kila Mtanzania mzalendo mwenye mapenzi na nchi yake aweze kusikia harufu mbaya, harufu mbaya ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Inafaa kila mtu mwenye akili timamu ahoji ujumbe wa Kafulila kwenda India je kuliambatana na maafisa wa usalama taifa pamoja na takukuru kufuatilia kwa karibu majadiliano na makubaliano ya Kafulila na kama kulikua na kuzingatia maslahi mapana ya taifa na kutokuwepo kwa rushwa.
Kwa bahati mbaya taasisi nilizozitaja hapo juu ya pili ndio kinara wa Rushwa na ya kwanza ina kazi maalumu ya kulinda wezi na kuilinda ccm na viongozi wake huku vijana wao wakikaa baa na kutishia watu bastola.
Ni wasi wasi wangu kwamba gharama kubwa anayoitumia kafulila kudalalia PPP ni dhahiri kwamba anatumikia rushwa aliyopewa na hao mabepari uchwara na wanaolenga kuvuna rasilimali zetu kwa kipindi kifupi ambacho wanaamini namba one sio mwelewa wa kutosha juu ya mambo magumu na makubwa ya nchi hasa maeneo ya miradi mikubwa ya maendeleo.
Wenzetu huko duniani wametumia idara husika kupata taarifa sahihi na kuamua kumtia nguvuni bwana Adani hasa kwamba wenzetu wana taarifa za uhakika, hawkamati kwanza ndio uchunguzi uanze la hasha. Jirani zetu kenya baada ya kupata taarifa hizi maramoja wamefuta mikataba na huyu jamaa. Changamoto ni kwamba sisi kwa sababu ya rushwa na ujinga, tulibadilisha sheria zetu kwa ajili ya wawekezaji badala ya waekezaji kufuata sheria zetu ili kumjengea mwarabu wa DP njia ya kutumia rasilimali zetu, kwa sheria zinazotufunga sisi hutasikia tumbili akitamka neno wala kitika akibwabwaja neno. Tutakaa kimya na kumpigia debe chini chini ale hiyo tenda ya umeme na huku akitafuna Bandarini.
Shida inakuja kwamba hisa za Adani zimeshuka ghafla na speculators wameanza kutoa fedha zao kwenye soko la hisi mpaka jana imeshuka kwa 20 percent. Kinachoendelea ni kwamba ufanisi utakua zero, tukimfukuza atatushtaki tumlipe na baadae tuje tuwsingizie chadema. Taasisi za ndani zikifanya kazi kwa maslahi ya nchi na si maslahi ya ccm na kafulila tutafika mbali
Lucas Mwashambwa aisome kwenye faili lake mana anampiga debe kuliko angefanya Jesca Kishoa na ndugu
Pascal Mayalla utusaidie ni namna gani hizo taasisi nilizotaja zinaweza kutusaidia.
https://www.reuters.com/world/india...dicts-group-chairman-bribery-case-2024-11-21/