Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
- Thread starter
- #41
Asante sana Mkuu Dolphin T. Hakika tusipopiga kelele hata kwa njia hii hapa JF huyu atatumaliza. Kama ulivyosema TAKUKURU na TISS wako kwenye majukumu ya kujinufaisha wao binafsi. Hawa wa Vibastola wanaeleweka na lugha yao ya " Unajua Minani?" Hawa TAKUKURU sasa ni TAASISI YA KUDAI NA KUCHUKUA RUSHWA. hawana hata aibu. Kuna mwaka walifanya sherehe nadhani ya kuukaribisha mwaka kule Kigamboni, sasa kuna dada alizinguliwa na Kaka kwenye kazi zao huko nyuma. Inasemekana huyu kaka alizuia dada asiweze kuchukua rushwa kwa tajiri mmoja hela kubwa sana. Sasa dada akawa na bifu na huyu kaka. Siku ya kuukaribisha mwaka mpya ilikuwa ni hitimisho la kupumua yule kaka na ikawa mwanzo wa maisha mapya gerezani kwa yule dada bastola ilifanya yake kwa kaka wa watu. Kwahiyo hawa si watu wa kuaminika tena ilikuwa zamani. Kulinganisha zamani na sasa ukisoma Makala ya Pascal Mayalla jinsi Mkurugenzi wa TISS Mzee Emilio Mzena alivyo staafishwa utaona viongozi wetu walivyokuwa committed kufanya kazi. Leo hii hawa watu wa Taasisi hizi mbili si watu wema tena kwa taifa letu. Nikiikumbuka kesi ya Loliondo na Ngorongoro nalia machozi tu. Naamini ipo siku Tanzania itarudi kwenye ramani yake. Asante Dolphin T.Hili halifai kupingwa hata kidogo ingefaa kila Mtanzania mzalendo mwenye mapenzi na nchi yake aweze kusikia harufu mbaya, harufu mbaya ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Inafaa kila mtu mwenye akili timamu ahoji ujumbe wa Kafulila kwenda India je kuliambatana na maafisa wa usalama taifa pamoja na takukuru kufuatilia kwa karibu majadiliano na makubaliano ya Kafulila na kama kulikua na kuzingatia maslahi mapana ya taifa na kutokuwepo kwa rushwa.
Kwa bahati mbaya taasisi nilizozitaja hapo juu ya pili ndio kinara wa Rushwa na ya kwanza ina kazi maalumu ya kulinda wezi na kuilinda ccm na viongozi wake huku vijana wao wakikaa baa na kutishia watu bastola.
Ni wasi wasi wangu kwamba gharama kubwa anayoitumia kafulila kudalalia PPP ni dhahiri kwamba anatumikia rushwa aliyopewa na hao mabepari uchwara na wanaolenga kuvuna rasilimali zetu kwa kipindi kifupi ambacho wanaamini namba one sio mwelewa wa kutosha juu ya mambo magumu na makubwa ya nchi hasa maeneo ya miradi mikubwa ya maendeleo.
Wenzetu huko duniani wametumia idara husika kupata taarifa sahihi na kuamua kumtia nguvuni bwana Adani hasa kwamba wenzetu wana taarifa za uhakika, hawkamati kwanza ndio uchunguzi uanze la hasha. Jirani zetu kenya baada ya kupata taarifa hizi maramoja wamefuta mikataba na huyu jamaa. Changamoto ni kwamba sisi kwa sababu ya rushwa na ujinga, tulibadilisha sheria zetu kwa ajili ya wawekezaji badala ya waekezaji kufuata sheria zetu ili kumjengea mwarabu wa DP njia ya kutumia rasilimali zetu, kwa sheria zinazotufunga sisi hutasikia tumbili akitamka neno wala kitika akibwabwaja neno. Tutakaa kimya na kumpigia debe chini chini ale hiyo tenda ya umeme na huku akitafuna Bandarini.
Shida inakuja kwamba hisa za Adani zimeshuka ghafla na speculators wameanza kutoa fedha zao kwenye soko la hisi mpaka jana imeshuka kwa 20 percent. Kinachoendelea ni kwamba ufanisi utakua zero, tukimfukuza atatushtaki tumlipe na baadae tuje tuwsingizie chadema. Taasisi za ndani zikifanya kazi kwa maslahi ya nchi na si maslahi ya ccm na kafulila tutafika mbali Lucas Mwashambwa aisome kwenye faili lake mana anampiga debe kuliko angefanya Jesca Kishoa na ndugu Pascal Mayalla utusaidie ni namna gani hizo taasisi nilizotaja zinaweza kutusaidia. https://www.reuters.com/world/india...dicts-group-chairman-bribery-case-2024-11-21/