Heshima sana wsnajamvi.
Kuna utaratibu wa hila na laghai za kila aina ambazo sijui chanzo chake au kusudio lake.
Huyu Kafulila kila uchao utasikia kasema hili mara kasema lile.
Ukitazama nyuzi kuhusu Kafulila hasa JF nadhani kuna kundi la watu pengine wanalipwa au yeye mwenyewe Kafulila kaamua kutuweka busy bila sababu za msingi.
Jadili hoja, usijadili mtoa hoja.
Ukimjadiki sana mtoa hoja, badala ya hoja, unajiingiza katika mtego wa kufanya ad hominem logical fallacy.
Sawa, Kafulila anaweza kuwa na ajenda yake, lakini unganisha basi anachoandika na ajenda yake usimshambulie jumlajumla tu.
Kwani Kafulila akifundisha mambo muhimu ya uchumi na PPP mambo hayo yataacha kuwa muhimu kwa sababu yamefundishwa na Kafulila tu?
JF haina limit ya mtu ku post.
Hata wewe unaruhusiwa ku post kila siku. Hiyo ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu.
Binafsi nimependa hoja fulani anazowasilisha bila kujali nani anawasilisha.
Hoja kama ya population bomb Tanzania aliyoisema ni hoja muhinu sana, na watu hawaisemi vya kutosha.
Sasa mtu akiiongelea utamlaumu vipi huyu anaongea sana wakati hoja ni muhimu na haiongelewi inavyotakiwa?
Kwenye hili la population mimi naona Kafulila peke yake hatoshi, tunahitaji watu zaidi waliongelee na kuliwekea mkakati wa kitaifa. Namshukuru sana kuliangazia jambo muhimu, jambo ambalo kwa kiasi ni unpopular, lakini kalisema vizuri.
Kafulila anachofanya ni kizuri, kwa sababu anaweka rekodi ya mawazo yake public watu wajue anafikiri nini.
Hili si tatizo. Tatizo ni watu wasioandika mambo ya uchambuzi.
Tatizo lingine ni pale unapoona mtu anayeandika uchambuzi ni tatizo.
Kama una tatizo na uchambuzi wake, pinga hoja kwa hoja. Kaandika mengi sana unayoweza kuyachambua na wewe.
Usihoji haki ya mtu kutoa hoja.