Kafulila: Rais Mkapa alijutia kuiua PSRC Parastatal Sector Reform Commission, PPP haiuzi Mali za Umma bali inazilinda kwa kipindi chote cha mkataba

Yaani uchukue nchi nzima?
Sijamaanisha hivyoo 😃😃😃

Ni kama ile msemo 'Tuanze na Mungu'.......

Kuna projekti ingefaa sana ifanywe ki PPP ina manufaa kwa wote lakini gharama za kuanza ni kubwa mnooo
 
Kwahiyo Nini kifanyike?
 
View attachment 3140086
View attachment 3140340
Hiki ndicho alichoandika Director wa PPP Tanzania Bw. David Kafulila huko kwenye akaunti yake ya X zamani tweeter.

Mkurugenzi huyo ameandika haya ili kuwatoa hofu wanaodhani huenda nchi yetu ikapata hasara ya mali na fedha kwa kuingia Ubia na Sekta binafsi toka ndani au nje ya Tanzania.

KAFULILA anarejelea Serikali ya awamu ya tatu Chini ya Hayati Rais Dkt. Benjamin Mkapa ambae katika kitabu chake Cha "My Life My Purpose " anasema baada ya kuuza mali za Umma kwa ubinafsishaji yakiwemo mashirika makubwa kama NBC kwa kupitia PSRC yaani Parastatal Sector Reform Commission anakiri alifanya makosa kuifuta tume hiyo ili ifanye ufuatiliaji wa mali zake zote ilizozifanyia ubinafshaji jambo lililozaa watu kuchukua mali za umma na kuzibadilishia matumizi, kukopea benki na uharibifu mwingine mwingi.

Kafulila anasema kwenye PPP Serikali na Sekta binafsi watamiliki mradi kwa pamoja na Serikali itakuwa ndio mwangalizi mkuu wa mradi kwa muda wote wa Mkataba na hii ndio tofauti kati ya Ubinafsishaji wa kipindi cha awamu ya tatu na Ubinafsishaji huu wa awamu ya sita kwa njia salama ya PPP.

Kafulila anasema PPP haiuzi mali za umma kama ilivyokuwa kwa PSRC bali inakodisha kwa kipindi maalum na baada kukodisha Serikali haiondoki kwenye mradi kwa kipindi chote cha Mkataba.

Na kwa ile miradi mipya itakayojengwa kwa Ubia kama zile Hosteli pale CBE baada ya muda wa Ubia kuisha miradi ile inarudi kuwa mali ya Serikali kwa asilimia 100.

Hata hivyo, ingawa haimaanishi Ubinafsishaji wa awamu ya tatu lilikuwa ni jambo baya hapana kwani ilikuwa ni njia sahihi ya kujenga Uchumi wa kisasa "modern economy" lakini matatizo hayawezi kuisha kabisa ila uamuzi wa Mzee Benjamin Mkapa wa ubinafshaji umekuwa na faida nyingi kuliko hasara Leo.

Pia soma Kwani Tulifeli vipi kwenye Ubinafsishaji wa Awamu ya 2 hadi Tufaulu sasa kwenye PPP ya David Kafulila?
Hongera sana mwandishi kwa ufafanuzi mzuri sana
 
Kwahiyo Nini kifanyike?
Project zile za kijamii mfano Sahili Movies zifanywe ki PPP.

Bila kuzisahau tafiti. Mfano za tiba asili kutokana na unyeti wake katika medical security ya nchi zifanywe ki PPP pia.

Chochote tu ambacho mtu ana wazo ambalo faida yake kwa jamii ni kubwa sana, wazo linalobiasharishika lakini gharama za kuanza ni kubwa sana basi lifanyike ki Puplic na huyo Private kama Partners. Nchi ina misuli mikubwa so inaweza kuingia riski kubwa zaidi. Pia inao mkono mrefu wa dola. Perfect kwa kuwa baba wa miradi.
 
View attachment 3140086
View attachment 3140340
Hiki ndicho alichoandika Director wa PPP Tanzania Bw. David Kafulila huko kwenye akaunti yake ya X zamani tweeter.

Mkurugenzi huyo ameandika haya ili kuwatoa hofu wanaodhani huenda nchi yetu ikapata hasara ya mali na fedha kwa kuingia Ubia na Sekta binafsi toka ndani au nje ya Tanzania.

KAFULILA anarejelea Serikali ya awamu ya tatu Chini ya Hayati Rais Dkt. Benjamin Mkapa ambae katika kitabu chake Cha "My Life My Purpose " anasema baada ya kuuza mali za Umma kwa ubinafsishaji yakiwemo mashirika makubwa kama NBC kwa kupitia PSRC yaani Parastatal Sector Reform Commission anakiri alifanya makosa kuifuta tume hiyo ili ifanye ufuatiliaji wa mali zake zote ilizozifanyia ubinafshaji jambo lililozaa watu kuchukua mali za umma na kuzibadilishia matumizi, kukopea benki na uharibifu mwingine mwingi.

Kafulila anasema kwenye PPP Serikali na Sekta binafsi watamiliki mradi kwa pamoja na Serikali itakuwa ndio mwangalizi mkuu wa mradi kwa muda wote wa Mkataba na hii ndio tofauti kati ya Ubinafsishaji wa kipindi cha awamu ya tatu na Ubinafsishaji huu wa awamu ya sita kwa njia salama ya PPP.

Kafulila anasema PPP haiuzi mali za umma kama ilivyokuwa kwa PSRC bali inakodisha kwa kipindi maalum na baada kukodisha Serikali haiondoki kwenye mradi kwa kipindi chote cha Mkataba.

Na kwa ile miradi mipya itakayojengwa kwa Ubia kama zile Hosteli pale CBE baada ya muda wa Ubia kuisha miradi ile inarudi kuwa mali ya Serikali kwa asilimia 100.

Hata hivyo, ingawa haimaanishi Ubinafsishaji wa awamu ya tatu lilikuwa ni jambo baya hapana kwani ilikuwa ni njia sahihi ya kujenga Uchumi wa kisasa "modern economy" lakini matatizo hayawezi kuisha kabisa ila uamuzi wa Mzee Benjamin Mkapa wa ubinafshaji umekuwa na faida nyingi kuliko hasara Leo.

Pia soma Kwani Tulifeli vipi kwenye Ubinafsishaji wa Awamu ya 2 hadi Tufaulu sasa kwenye PPP ya David Kafulila?
Alijutia wapi???
Mbona kwenye kitabu chake hajaiweka hii.
 
Kijana pekee anayevuta matumaini ya Vijana mtaani kuwa na imani na CCM Kwa Sasa ni Kafulila
 
Back
Top Bottom