Kafulila: Sera ya UBWABWA ya CHAUMA na Mzee Hashimu Rungwe iingizwe kwenye Dira yetu ya Taifa ya Maendeleo ya 2025-2050 na sababu ni hizi…

Kafulila nakubaliana na wewe ila haya mambo ya lishe yawekwe kwenye ngazi ya familia sio ngazi ya Kitaifa
 
Kumbe Mzee Rungwe alikuwa anaanisha?
Ila Utapiamlo Tanzania sio tatizo kubwa
 
Imeanza lini Mkuu?
Kila mwaka Kuna maadhimisho ya Lishe na kupiga vita utapiamlo Nchini .

Halmashauri zote hii ni ajenda ya kudumu kama Ukimwi.

Mwisho wakati Chauma Wanaleta mambo ya Ubwabwa haikuwakwa mantiki ya Lishe Bali chakula Kwa Watoto waoashinda kutwa nzima bila kula akisema wao wakati wanasoma walikula shule na ni kweli hata Mimi tumekula shule na uji Juu ila miaka ya katikati hapo huo utaratibu ulifutwa.
 
Yes nakumbuka huu utaratibu ulifutwa
 
Ubwabwa huu unatia njaa aisee
 
Concept ya Mzee Rungwe ilikuwa kusisitiza lishe maana tatizo kuu la watanzania ni ukosefu wa akili smart ambao chanzo chake ni wengi kukosa lishe bora utotoni.
 
Ila Kafulila huwa akili kubwa sana,
Hili jambo kama litaingia kwenye Dira yetu na kutungiwa Sheria inakuwa ni manufaa sana kwa familia hasa Masikini kabisa wa kipato na mali
 
Huu wali ukimpa mtoto atasoma kweli au ndio kusinzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…