Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
2,128
Reaction score
1,896
IMG-20240612-WA0089(1).jpg

CEO wa PPP Bwana David Kafulila katika Ukurasa wake wa tweeter ( X ) ameisifu Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ndio nchi pekee inayokopa ndani kwa riba ndogo kuliko nchi nyingi za Africa.

Kafulila anasema Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakopa T-bills kwa asilimia 5 lakini wenzetu uchumi wao ndani ni hoi ndio sababu Riba zao kwenye T-bills ziko juu mafano Msumbiji ni asilimia 17 Kenya ni asilimia 16, Malawi ni Asilimia 16, Zambia ni Asilimia 10,Namibia ni asilimia 9,Uganda ni asilimia 9 na Africa ya kusini ni asilimia 8 hiki ni kielelezo Cha uimara wa Uchumi wetu ndani katika ukanda wa Africa.

Wakati mnaendelea kumtukana msisahau pia kuwaambia hao Wananchi kuwa ni yeye pekee ndio aliyejenga unafuu wa maisha kwa watu wake katika ukanda mzima wa Africa na baadhi ya ushahidi ni hizo taarifa za David Kafulila huko tweeter ( X )

IMG-20240613-WA0002.jpg
 
mbona mnamtetea sana huyo mtu ila hali halisi inajionyesha mtaani halafu tuna uhakika gani kama 5% kweli au ndio zile habari za kuambizana tuko uchumi wa kati.....

ukiona mtu anatetewa sana kuna mawili uwezo mdogo au watetezi wana kafungu kao
 
 Ephen: Naomba unikopeshe laki 1, nitakurudishia wiki ijayo

Rafiki: kama unataka laki 1 riba ni 50% hivyo utanilipa 150,000

Ephen: Turahisishe mambo nipe laki 1, mimi nakupa Hati ya kiwanja cha familia yetu halafu wiki ijayo nakupa hela yako bila riba.

Rafiki: Sio kweli! Nachukua kiwanja na utanilipa riba ya 10%= 110,000

Ephen: Sawa! Asante kwa wema wako
 
Kachukue taarifa za BOT mkuu hili liko hivyo tunakopa kwa 5% toka kwa watu binafsi na mashika mbalimbali
 
Hakuna Mtanzania Mtanzania anaweza akakubali hili
 
View attachment 3016052
CEO wa PPP Bwana David Kafulila katika Ukurasa wake wa tweeter ( X ) ameisifu Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ndio nchi pekee inayokopa ndani kwa riba ndogo kuliko nchi nyingi za Africa.

Kafulila anasema Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakopa T-bills kwa asilimia 5 lakini wenzetu uchumi wao ndani ni hoi ndio sababu Riba zao kwenye T-bills ziko juu mafano Msumbiji ni asilimia 17 Kenya ni asilimia 16, Malawi ni Asilimia 16, Zambia ni Asilimia 10,Namibia ni asilimia 9,Uganda ni asilimia 9 na Africa ya kusini ni asilimia 8 hiki ni kielelezo Cha uimara wa Uchumi wetu ndani katika ukanda wa Africa.

Wakati mnaendelea kumtukana msisahau kuwaambia Wananchi kuwa ni yeye pekee aliyejenga unafuu wa maisha ya watu katika ukanda mzima wa Africa na baadhi ya ushahidi ni hizo taarifa za David Kafulila huko tweetwr.

View attachment 3016048
Haya mambo ya kulingania ni ya kijinga sana
 
Kachukue taarifa za BOT mkuu hili liko hivyo tunakopa kwa 5% toka kwa watu binafsi na mashika mbalimbali
na hali ipoje mtaani tunakopa kuendesha serikali alafu walipaji ni wananchi.... ogopa sana nchi yenye vyanzo lukuki vya pesa kwenda kukopa na kuanza kujilinganisha asilimia na nchi jirani ogopa sana......

huwezi ukawa na mali ukashindwa kuitumia alafu ukaenda kukopa kausha damu na kuwadamganya wananchi 5% ni ujinga...
 
Hizi Tbonds tunazikopa hapa hapa ndani ya nchi sio nje mkuu kuwa na amani.
 
 Ephen: Naomba unikopeshe laki 1, nitakurudishia wiki ijayo

Rafiki: kama unataka laki 1 riba ni 50% hivyo utanilipa 150,000

Ephen: Turahisishe mambo nipe laki 1, mimi nakupa Hati ya kiwanja cha familia yetu halafu wiki ijayo nakupa hela yako bila riba.

Rafiki: Sio kweli! Nachukua kiwanja na utanilipa riba ya 10%= 110,000

Ephen: Sawa! Asante kwa wema wako
Mada ifungwe hapa hapa. Akili mtu wangu
 
Sio Sifa ila hata familia yako kama unataka kuwa tajiri kuwazidi wengine lazima ukope, Bakresa pia analoan kibao kwenye mabenki
kukopa sio tatizo matumizi ndio hatuelewi hapo tushakopa pesa kibao riba zinasubiriwa ila hakuna cha maana jiulize zile 190+b za kununua magari mapya ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya hakukua na sehemu nyingine ya kupeleka hiyo pesa unanunulia kiongozi gari wakati analotumia bado linauwezo wa kuhudumu
 
Naona Kafulila anautafuta ubunge hiyo 2025 kwa nguvu zote, kamwaga chawa mitandaoni. Unfortunately wapiga kura wake wako kigoma hata hawayajui hayo, alafu kuna kihunzi cha wajumbe.

Au ndio anaitaka nafasi ya Zuhura kwa kubwabwaja takwimu za uongo??
Kwani Ubunge ni kosa mkuu? Acha akajaribu bahati yake.
 
hivi ni Kwa nini tunashabikia sana kukopa? Hii sio sifa nzuri hata kidogo... sijui Ni lini tutatoka ktk hizi habari za tunakopeshwa, riba ndogo, ... ni utumwa kudaiwa, fedheha ukimuona mdaiwa wako, Na karaha Kwa mfuatiliaji wa madeni .
Ifike Mahali viongozi wetu waje Na mpango wa ni namna gani tutakuwa debt free sisi Kama Nchi , sio kila siku tunakopa, imekuwa Kausha damu inadumaza sana akili... tunaishi kama digidigi... tumechoka Na kudhihakiwa Na mikopo. Viongozi amkeni...
 
Back
Top Bottom