Hana facts zozote ni mtu wa kuokoteza vitaarifa bila ya kuwa na uwezo wa kuchambua kitaalam.
Sidhani kama anaelewa hata hiyo business ya treasury bills and bonds inavyofanya kazi. Treasury bills ni mnada. Kunapokuwa na opportunities chache za uwekezaji au faida ndogo sana ukiweka pesa yako bank, wengi wenye hela mnaamua kuikopesha Serikali ambapo ni mkopo mnaipa serikali kwa vipindi vifupi vifupi kwa riba inayotegemea mnada unavyoamua.
Kunapokuwa na wengi wanaotaka kuikopesha Serikali, riba inashuka. Hivyo kwa Tanzania kuwa na riba ndogo kwenye treasury bills kunaashiria fursa chache za uwekezaji au mazingira mabaya ya uwekezaji, na hivyo mtu anaona aheri aikopeshe Serikali yenyewe ili kuepuka usumbufu unaosababishwa na Serikali yenyewe kwenye uwekezaji. Na kwa kuwa mpo wengi, riba inashuka. Kwenye biashara ya treasury bills, hakuna TRA, OSHA, TBS wala tozo.
Hizo nchi zenye riba kubwa ina maana wenye hela wanaona wana uwezo wa kutengeneza faida kubwa zaidi kwa kuwekeza maeneo mengine kuliko faida wanayoweza kuipata kwa kuikopesha Serikali. Hivyo wachache walioamua kuikopesha serikali, wanaikopesha kwa riba kubwa.