Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

kukopa sio tatizo matumizi ndio hatuelewi hapo tushakopa pesa kibao riba zinasubiriwa ila hakuna cha maana jiulize zile 190+b za kununua magari mapya ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya hakukua na sehemu nyingine ya kupeleka hiyo pesa unanunulia kiongozi gari wakati analotumia bado linauwezo wa kuhudumu
Sasa unataka watembee kwa miguu?
 
hivi ni Kwa nini tunashabikia sana kukopa? Hii sio sifa nzuri hata kidogo... sijui Ni lini tutatoka ktk hizi habari za tunakopeshwa, riba ndogo, ... ni utumwa kudaiwa, fedheha ukimuona mdaiwa wako, Na karaha Kwa mfuatiliaji wa madeni .
Ifike Mahali viongozi wetu waje Na mpango wa ni namna gani tutakuwa debt free sisi Kama Nchi , sio kila siku tunakopa, imekuwa Kausha damu inadumaza sana akili... tunaishi kama digidigi... tumechoka Na kudhihakiwa Na mikopo. Viongozi amkeni...
Mkuu Dunia yote inanuka madeni lazima na sisi tukope ili kuendelea
 
Kachukue taarifa za BOT mkuu hili liko hivyo tunakopa kwa 5% toka kwa watu binafsi na mashika mbalimbali
Mkuu angalia usije ukakurupuka wenye akili wakakuona upstairs una makamasi kama ya huyo tumbiri anayetafuta sifa za kisiasa.
BOT inapo issue T-bill kwa umma katika riba kubwa au ndogo inategemeana na lengo la kiuchumi ambalo Serikali inataka kulifanikisha.hapo issue sio riba kubwa au ndogo inategemeana na jambo la kiuchumi lililopelekea Serikali ku offer hizo hati fungani.
Kenya anaweza offer 16% lakini lengo Lake ni ku curb inflation,Tanzania unaweza ku offer 5% but lengo lake ni kupata pesa kupeleka kwenye uchaguzi,Namibia anaweza ku offer 9% a lengo lake anataka kupata pesa apeleke kwenye kujenga mradi.
 
Haya ni matokeo ya mnada wa jana June 12 - Average rate ilikuwa 6.75

1718253181232.png
 
Mkuu angalia usije ukakurupuka wenye akili wakakuona upstairs una makamasi kama ya huyo tumbiri anayetafuta sifa za kisiasa.
BOT inapo issue T-bill kwa umma katika riba kubwa au ndogo inategemeana na lengo la kiuchumi ambalo Serikali inataka kulifanikisha.hapo issue sio riba kubwa au ndogo inategemeana na jambo la kiuchumi lililopelekea Serikali ku offer hizo hati fungani.
Kenya anaweza offer 16% lakini lengo Lake ni ku curb inflation,Tanzania unaweza ku offer 5% but lengo lake ni kupata pesa kupeleka kwenye uchaguzi,Namibia anaweza ku offer 9% a lengo lake anataka kupata pesa apeleke kwenye kujenga mradi.
Nadhani hoja ni rates Wala sio matumizi, Kumbuka unapokopa kwa 17% anayeumia ni Mwananchi,

Unadhani Mwananchi anauelipa riba ya 17% maumivu yake ni sawa na yule anayelipa riba 5%?
 
mbona mnamtetea sana huyo mtu ila hali halisi inajionyesha mtaani halafu tuna uhakika gani kama 5% kweli au ndio zile habari za kuambizana tuko uchumi wa kati.....

ukiona mtu anatetewa sana kuna mawili uwezo mdogo au watetezi wana kafungu kao
Mtaani kwako kukoje kulinganisha na lini? Leta majibu
 
ficha ujinga saa hizi walipo wana magari mazuri tu sasa hayo mapya ya nini labda na hiyo hela iingeweza fanya mambo mangapi yanayogusa moja kwa moja mwananchi?
Magari hayo yalinunuliwa na Kikwete miaka 10 iliyopita yamechoka naamini
 
hivi ni Kwa nini tunashabikia sana kukopa? Hii sio sifa nzuri hata kidogo... sijui Ni lini tutatoka ktk hizi habari za tunakopeshwa, riba ndogo, ... ni utumwa kudaiwa, fedheha ukimuona mdaiwa wako, Na karaha Kwa mfuatiliaji wa madeni .
Ifike Mahali viongozi wetu waje Na mpango wa ni namna gani tutakuwa debt free sisi Kama Nchi , sio kila siku tunakopa, imekuwa Kausha damu inadumaza sana akili... tunaishi kama digidigi... tumechoka Na kudhihakiwa Na mikopo. Viongozi amkeni...
Kukopa na kujenga miradi ndio maisha ya Dunia mkuu wangu, It is inevitable
 
View attachment 3016052
Kafulila katika Ukurasa wake wa tweeter (X) ameisifu Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ndio nchi pekee inayokopa ndani kwa riba ndogo kuliko nchi nyingi za Africa.

Kafulila anasema Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakopa T-bills kwa 5% wenzetu uchumi wao ni hoi ndio sababu Ripa ziko juu mafano Msumbiji 17% Kenya 16%,Malawi 16% Zambia 10%,Namibia 9%,Uganda 9% SA 8% hili ni kielelezo Cha uimara wa Uchumi wetu katika ukanda wa Africa.

View attachment 3016048
Hebu chukua hesabu rahisi si Ina maana kama nchi hizi zikiuza hati fungani kwa mtu wa ndani mathalani" tutumie Euro"1000 zikiiva Tanzania itarejedha 1000+(1000x5%)=€1,050,Kenya=1,160,SA=1,
080,Msumbiji=1,170,Malawi=1,160,Zambia=1,100,Namibia=1,090.Sasa kama hizi hesabu ni sawa ni wapi wakopeshaji wa ndani wanafaidi!na tafsiri yake ni nini.
 
Hoja hapa ni rahisi Mkuu,

Serikali inaangalia unafuu kwa wananchi walio wengi ambao ni masikini na walala hoi.

Wanaonunua hizi bonds ni taasisi kubwa au Matajiri wakubwa,

Sasa huwezi kunufaisha Matajiri ukawaumiza walala hoi,

Ndio maana Kafulila anamsifu Mama ni Kwa dhana kama hizi.
 
View attachment 3016052
CEO wa PPP Bwana David Kafulila katika Ukurasa wake wa tweeter ( X ) ameisifu Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ndio nchi pekee inayokopa ndani kwa riba ndogo kuliko nchi nyingi za Africa.

Kafulila anasema Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakopa T-bills kwa asilimia 5 lakini wenzetu uchumi wao ndani ni hoi ndio sababu Riba zao kwenye T-bills ziko juu mafano Msumbiji ni asilimia 17 Kenya ni asilimia 16, Malawi ni Asilimia 16, Zambia ni Asilimia 10,Namibia ni asilimia 9,Uganda ni asilimia 9 na Africa ya kusini ni asilimia 8 hiki ni kielelezo Cha uimara wa Uchumi wetu ndani katika ukanda wa Africa.

Wakati mnaendelea kumtukana msisahau pia kuwaambia hao Wananchi kuwa ni yeye pekee ndio aliyejenga unafuu wa maisha kwa watu wake katika ukanda mzima wa Africa na baadhi ya ushahidi ni hizo taarifa za David Kafulila huko tweeter ( X )

View attachment 3016048
Sisi tunawapa na rasilimari pori,na miradi itakayofanyika wao wanapewa kipaombele,huwezi pewa kitu if there is no return of investment hakuna hio formula duniani
 
View attachment 3016052
CEO wa PPP Bwana David Kafulila katika Ukurasa wake wa tweeter ( X ) ameisifu Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ndio nchi pekee inayokopa ndani kwa riba ndogo kuliko nchi nyingi za Africa.

Kafulila anasema Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakopa T-bills kwa asilimia 5 lakini wenzetu uchumi wao ndani ni hoi ndio sababu Riba zao kwenye T-bills ziko juu mafano Msumbiji ni asilimia 17 Kenya ni asilimia 16, Malawi ni Asilimia 16, Zambia ni Asilimia 10,Namibia ni asilimia 9,Uganda ni asilimia 9 na Africa ya kusini ni asilimia 8 hiki ni kielelezo Cha uimara wa Uchumi wetu ndani katika ukanda wa Africa.

Wakati mnaendelea kumtukana msisahau pia kuwaambia hao Wananchi kuwa ni yeye pekee ndio aliyejenga unafuu wa maisha kwa watu wake katika ukanda mzima wa Africa na baadhi ya ushahidi ni hizo taarifa za David Kafulila huko tweeter ( X )

View attachment 3016048

Ujinga kabisa!! Kwa ujinga kama huu, naye Kafulila anajiona ni muelewa wa masuala ya uchumi!!

Nani alikuambia kuwa serikali kukopa treasury bills kwa riba ndogo kunaashiria uchumi mzuri?

Kwanza kiuhalisia ni kuwa hizo nchi ambazo serikali inawakopa wananchi wake kwa treasury bills zenye riba kubwa, zinawanufaisha zaidi wananchi wao kuliko wananchi wa Tanzania wanaoikopesha Serikali kwa riba ndogo zaidi.

Lakini jambo jingine, hizo treasury bills za Tanzania ni za muda gani, na hizo za nchi nyingine ni za muda gani? Mnaweka tu sweeping statements kwa mambo msiyoyajua sawasawa.
 
Back
Top Bottom