Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Mkuu angalia usije ukakurupuka wenye akili wakakuona upstairs una makamasi kama ya huyo tumbiri anayetafuta sifa za kisiasa.
BOT inapo issue T-bill kwa umma katika riba kubwa au ndogo inategemeana na lengo la kiuchumi ambalo Serikali inataka kulifanikisha.hapo issue sio riba kubwa au ndogo inategemeana na jambo la kiuchumi lililopelekea Serikali ku offer hizo hati fungani.
Kenya anaweza offer 16% lakini lengo Lake ni ku curb inflation,Tanzania unaweza ku offer 5% but lengo lake ni kupata pesa kupeleka kwenye uchaguzi,Namibia anaweza ku offer 9% a lengo lake anataka kupata pesa apeleke kwenye kujenga mradi.
Kwa nini unataka kuonesha kwamba Tanzania tunafanya hivyo Kwa Ajili ya uchaguzi? Je miaka yote hatufanyi hivyo? Miaka yote kuna uchaguzi?

Kwani ukipongeza uimara wa Sera za Samia RC aliyetumbuliwa atakupitia? Acha chuki za kijinga wewe.

Hata sovereign rating agency zote zimeiwwka Tanzania kwenye alama.ya B+ kutoka B- Kwa sababu ya stable macroeconomic policies.
 
RC aliyetumbuliwa atakupitia🤣🤣
 
Huyu wetu mambo ya asilimia anayajua au anadondosha saini tu

Refer to teuzi ya marehemu
 
Kama wanakopa kwa riba ya 5%, Kwanini wauze bonds za serikali kwa riba ya 15%?

Uongo mwingine hata haujaenda shule.

Una sehemu ya kukopa kwa asilimia 5 kweli uta issue Bonds za kukopa kwa asilimia 15?
 
Kuna kitu hujakifahamu vizuri mkuu,

Mwisho wa Siku deni litalipwa na Wananchi,

Unadhani mwananchi atakayerejesha 17% na huyu wa 5% nani anafaida,?

Watu wanawekeza kwenye 5% ndio Maana zinauzwa.

Kinachoendeleza nchi, riba ya madeni ina effect ndogo sana. Kilicho muhimu kwenye uchumi ni uchangamfu wa uchumi.

Uchumi uliosinyaa, hata ukaambiwa mkopo hauna riba, unaweza kushindwa kulipa, wakati kwenye uchumi uliochangamka, deni hata lenye riba kubwa linaweza kulipwa bila ya tatizo lolote, na bila ya kuleta maumivu kwa wananchi.

Nikupe Shule Fupi:
Fikiria nchi 2 ambazo zina idadi sawa ya watu, let say 10m wenye uwezo wa kufanya kazi. Moja, asilimia 80 wapo employed. Nyingine watu asilimia 10 tu wapo employed. Yenye 80% employed, average income ya kila mtu kwa mwaka ni sh 10m. Ina maana pato lao la jumla ni 10m × 8m = trilioni 80.
Hii nyingine yenye 10% employed, ni 10m×1m = 10trillion.

Hawa wenye 80% employed wakichukua mkopo wa 100 billion wenye riba ya 10%, riba yao itakuwa 10 billion. Na wale wa 10% employed wakichukua mkopo wa 100 bilioni wenye riba ya 5%, riba itakuwa 5 bilioni. (Cheza na simple arithmetics). Lakini katika kulipa, wale ambao ni 80% employed, kila mwajiriwa atalipa 0.0125%; wakati wale ambao only 10% employed, kila mwajiriwa atalipa 0.05%, yaani karibia mara 5 ya nchi ambayo watu wake wengi wana ajira, na wamechukua mkopo wenye riba mara 2 ya hawa wenye matatizo ya ajira.

Uchumi siyo kitu rahisi kama Tumbili anavyotaka kuwadanganya watu.
 
Kwanza Ukiwa mbumbumbu wa Uchumi lazima ushangae.

Ila Iko hivi Ili uendeshe uchumi kukopa na kukopesha ni lazima ,Ili uchumi ukue kukopa na kukopesha ni lazima.

Kiufupi kukopa na kukopesha ni economic tool,wachumi wanajua how economic regulation is dome.

Mwisho Hakuna Nchi ambayo haikopp hapa Duniani,haipo hata hao wanaotoa mikopo hukopa pia.
Kwa hiyo ni lazima tukope ili tufanye mambo yetu... mbona hii theory ya Thaksinomics ndio iliyomaliza madeni ya Thailand na kuondoa umaskini na sisi bado tupo tupo tu au hili nalo ni kuwa mbumbumbu wa uchumi?
 
Kachukue taarifa za BOT mkuu hili liko hivyo tunakopa kwa 5% toka kwa watu binafsi na mashika mbalimbali
Hili ni wazo la kipuuzi sana, wananuaji wa hizi bills ni banks, kama wao wananunua kwa 5% depositors watapata loyalty ya 1%, msumbiji their far better buying ni 17% bank depositors wakipewa 10% will be great!
 
Naona Kafulila anautafuta ubunge hiyo 2025 kwa nguvu zote, kamwaga chawa mitandaoni. Unfortunately wapiga kura wake wako kigoma hata hawayajui hayo, alafu kuna kihunzi cha wajumbe.

Au ndio anaitaka nafasi ya Zuhura kwa kubwabwaja takwimu za uongo??
Mheshimiwa Kafulila hatafuti ubunge kwa nguvu bali ubunge ndio unaomtaka na kumtafuta yeye.ndio maana watanzania wanampigania sana katika kutaka kuona anaingia Bungeni hapo mwakani.hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa na uelewa wake mkubwa wa masuala mbalimbali
 
Kachukue taarifa za BOT mkuu hili liko hivyo tunakopa kwa 5% toka kwa watu binafsi na mashika mbalimbali
Hili ni wazo la kipuuzi sana, wananuaji wa hizi bills ni banks, kama wao wananunua kwa 5% depositors watapata loyalty ya 1%, msumbiji their far better buying ni 17% bank depositors wakipewa 10% will be great
 
Kwa hiyo ni lazima tukope ili tufanye mambo yetu... mbona hii theory ya Thaksinomics ndio iliyomaliza madeni ya Thailand na kuondoa umaskini na sisi bado tupo tupo tu au hili nalo ni kuwa mbumbumbu wa uchumi?
Ndio ,sio tuu ukope kufanya mamabo Yako Bali ni lazima kukopa na kukopesha Ili kuendesha uchumi.

Kwamba Thailand Haina Madeni ,Nchi ambayo Kila mwaka wanabadilisha Viongozi Kwa sababu ya Hali mbaya ya uchumi? Wacha kudanganywa ,weka facts hapa zinazosema Thailand Haina Madeni Ili twende sawa.

Mwisho kukopa sio lazima iwe Nje hata ndani lakini kukopa Ndani ni very risk Kwa sababu unapunguza mzunguko wa hela private sector n pia inaweza ongeza riba Kwa private sector
 
Hizo taarifa za upotoshaji zitakuwa na msaada gani kwa umma. Takwimu zake zaweza kuwa sawa, lakini tafsiri siyo sahihi kabisa.
Weka tafsiri sahihi ambayo ndio mantiki ya mtoa mada na Kafulira maana nimeona at ceteris Paribas hata Mimi sijaelewa alimaanisha nini japo tafsiri ya kiswahili uelekeo sahihi Iko sawa
 
Hili ni wazo la kipuuzi sana, wananuaji wa hizi bills ni banks, kama wao wananunua kwa 5% depositors watapata loyalty ya 1%, msumbiji their far better buying ni 17% bank depositors wakipewa 10% will be great!
Hoja yako yako iko kinyume chako,

Mfano Benki ikinunua bills za Tsh 100,000

Then mwisho italipwa TZS 100,000XO.O5=105,000

ILA BENKI WAO WANATOA PESA KWA 16%
 
Back
Top Bottom