Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Safi sana kijana
 
Kama OMO ipo kwanini tufulie sabuni ya kipande, hata kama ni wewe uncle
 
Ila lazima tukope kwa Malengo madhubuti
Wasiwasi wangu ni marejesho… hapo ndipo ilipo shughuli…sitaki tutape fedheha huko mbele ya safari tukisuasua kuilipa Kama siku za nyuma ilivyokuwa hadi Paris club ikatusamehe baadhi ya madeni miaka ile ya 1998-2000 ( Kama unakumbuka vizuru) hawa ngozi nyeupe naishi nao, nafanya kazi nao day in day out, wakikupa mkopo huwa ni mtego wa kuku-control… siku ukianza kulipa ndio utajua small prints zote za mkataba…
Mwisho - sisi Kama nchi tunakopa sana…hawa wenzetu huwezi sikia wanakopa kujenga Barbara maana barabara zao zinapitika siku 365 bila kujali hali ya hewa, suala la maji safi na salama- wamemalizana nalo pia, Kwa kweli na sisi tumalizane na baadhi ya mambo Kama Chakula, maji safi na salama, kipindu pindu, barabara, etc

Tuna vyanzo na rasimali za kutosha kutufanya sisi kuendelea bila mikopo ya masharti nafuu ya kulipwa baada ya mpaka 40…
Tuwe na research centres zetu kwenye Kila Nyanja zitakazo toa majibu ya nini kifanyike Katia mambo yote tunanayo hitaji Kama taifa…
Na tukiweza Hivyo ndio tunaweza toboa Kama akina South Korea, china, ulaya na America.

Kwa sasa bado Tupo kwenye trial and errors ktk Kila kitu … hakuna hata jambo moja tunaloweza jivunia isipokuwa ,” tunakopesheka”…
 
Serikali inayojivunia kukopa (haijalishi hata kama ni kwa riba nafuu) badala ya kujivunia ubunifu wa kuongeza/kukuza mapato kupitia hivyo hivyo vyanzo viliopo..... hiyo ni serikali mufilisi inayoongozwa na watu wasiokuwa na maarifa na wapenda shortcuts kwenye kila jambo
 
mbona mnamtetea sana huyo mtu ila hali halisi inajionyesha mtaani halafu tuna uhakika gani kama 5% kweli au ndio zile habari za kuambizana tuko uchumi wa kati.....

ukiona mtu anatetewa sana kuna mawili uwezo mdogo au watetezi wana kafungu kao
Sijui kwa nini wasiache hali halisi imtetee yenyewe, maana haya maneno yao yanapotea kama upepo.
 
mbona mnamtetea sana huyo mtu ila hali halisi inajionyesha mtaani halafu tuna uhakika gani kama 5% kweli au ndio zile habari za kuambizana tuko uchumi wa kati.....

ukiona mtu anatetewa sana kuna mawili uwezo mdogo au watetezi wana kafungu kao
huyu naye wamkumbukr tu aache kujiabisha
 
Mnajua kabisa wananchi hawataki mikopo. Endeleeni kushupaza mafuvu yenu yasiyo na brain.
 
Dah asali ni hatari sana wakuu, Kafulila huyu huyu yuko praise team sasaivi πŸ˜‚πŸ˜‚. Siasa shikamoo..
 
Mzee naona kazi uliyopewa ya kuutetea uchumi na kubariki mikopo inakaribia kukushinda, ni suala.la.muda.
 
Huwa nafurahi sana kuona takwimu kwenye mijadala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…