Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

SGR, SG mambo ni mazuri sana
 
Unalinganishaje Kenya na tz ,wakati uchumi Kenya wametuzidi , huyu kafulila mjinga sana
 
Huyu mwamba siku hz tangu apewe ulaji, anaimba kama shangingi/danga anasifia pipe ya bwana, "anayemlipa mpiga zumari, ndie huchagua wimbo" Ataimba Sana nyimbo za CCM,
 
Huyu mwamba siku hz tangu apewe ulaji, anaimba kama shangingi/danga anasifia pipe ya bwana, "anayemlipa mpiga zumari, ndie huchagua wimbo" Ataimba Sana nyimbo za CCM,
Mheshimiwa David Kafulila ni mtu msema kweli na anayezungumza kwa hoja na ushahidi.ndio maana hata wewe umeshindwa kupinga hoja zake na kuishia kupiga porojo tu hapa
 
mbona mnamtetea sana huyo mtu ila hali halisi inajionyesha mtaani halafu tuna uhakika gani kama 5% kweli au ndio zile habari za kuambizana tuko uchumi wa kati.....

ukiona mtu anatetewa sana kuna mawili uwezo mdogo au watetezi wana kafungu kao
Ugali ndugu yangu. Kwa sasa Tanzania asilimia kubwa ya watu ni machawa tu. Wamejitoa ufahamu. Tumbili pia anatafuta ugali wa watoto. Lazima asifie sana na ikiwezekana apate hata cheo zaid. Unaona Yule Prof wa masturbation kwa sasa ni wazir wa uchumi lakin hajui chochote kuhusu uchumi. Ila alisifia bandari.
 
NMB nawapenda sana
 
Nzuri sana hii hata hivyo
 
Huyu jamaa km ndo anakua mshauri wa rais mnaweza jikuta mmekopa na kuweka rehan kila kitu.Hivi kukopa ni sifa sijawahi mwelewa huyu tumbili.
Pepo wa madeni amemtawala inabidi tumuombee. Alipokuwa Upinzani alikuwa anaongea mambo ya maana, Sasa hv anashauri nchi iwekwe rehani. Lakini nahisi bado anataka nafasi kubwa zaidi. Acha apige debe. Kinachonishangaza eti anafananisha mikopo kwamba hatujakopa vya kutosha tuongeze tena. Anamdanganya mama yetu.
 
mbona mnamtetea sana huyo mtu ila hali halisi inajionyesha mtaani halafu tuna uhakika gani kama 5% kweli au ndio zile habari za kuambizana tuko uchumi wa kati.....

ukiona mtu anatetewa sana kuna mawili uwezo mdogo au watetezi wana kafungu kao
Porojo proMax
 
Hatutaki figures za kwenye karatasi tunataka kujua je watanzania wangapi wana uwezo wa kula milo mitatu kama zamani?wangapi wanauwezo wa kupata matibabu bila shida nk.Baada ya hapo substantiate na hizo treasury bills zenu
 
Siyo kila linganisho la "economic figure or indicator" hutupa tafsiri ya kuwa tupo vizuri kulinganisha na nchi nyingine. Ni vyema tafsiri pana ikawekwa nyuma ya hizi "relative numbers" ili watu wapate ufahamu wa kutosha.

Tukinukuu taarifa kutoka repoti ya IMF'

"The 364 days T-bill yields have improved to reach 7.2% as recorded on the auction conducted in mid-January 2024.. But unlike other T-bills, it has been transacted in all the past 23 auctions and with it being oversubscribed in most of the auctions"

Hapo ndipo Kafulila alipaswa kuijazia nyama hoja yake. Mlinganisho tu wa namba hautoshi kutupa mantiki ya kutosha. Bali ni tafsiri iliyopo nyuma ya namba ziliizotolewa, na kitu kilichopelekea kufikia kwa namba hizo ndicho hasa kitu muhimu katika mjadala.

Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi. Si kila kitu ni siasa, kwa kusifu na kuabudu ili kumpendezesha mkulu.
 
Siasa = Si hasa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…