Wasiwasi wangu ni marejesho… hapo ndipo ilipo shughuli…sitaki tutape fedheha huko mbele ya safari tukisuasua kuilipa Kama siku za nyuma ilivyokuwa hadi Paris club ikatusamehe baadhi ya madeni miaka ile ya 1998-2000 ( Kama unakumbuka vizuru) hawa ngozi nyeupe naishi nao, nafanya kazi nao day in day out, wakikupa mkopo huwa ni mtego wa kuku-control… siku ukianza kulipa ndio utajua small prints zote za mkataba…
Mwisho - sisi Kama nchi tunakopa sana…hawa wenzetu huwezi sikia wanakopa kujenga Barbara maana barabara zao zinapitika siku 365 bila kujali hali ya hewa, suala la maji safi na salama- wamemalizana nalo pia, Kwa kweli na sisi tumalizane na baadhi ya mambo Kama Chakula, maji safi na salama, kipindu pindu, barabara, etc
Tuna vyanzo na rasimali za kutosha kutufanya sisi kuendelea bila mikopo ya masharti nafuu ya kulipwa baada ya mpaka 40…
Tuwe na research centres zetu kwenye Kila Nyanja zitakazo toa majibu ya nini kifanyike Katia mambo yote tunanayo hitaji Kama taifa…
Na tukiweza Hivyo ndio tunaweza toboa Kama akina South Korea, china, ulaya na America.
Kwa sasa bado Tupo kwenye trial and errors ktk Kila kitu … hakuna hata jambo moja tunaloweza jivunia isipokuwa ,” tunakopesheka”…