Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Nimekudharau sana unaposema Mh Kafulila hawezi kufanya uchambuzi wa masuala ya kiuchumi na kwamba anakariri habari za kwenye magazeti. Kila mtanzania anafahamu uwezo mkubwa sana na uelewa wa masuala ya uchumi. Kila mtu ameona kwa macho na kusikia kwa masikio yake namna Mheshimiwa Kafulila anavyochambua na kuelezea kwa undani na kina masuala mbalimbali ya uchumi kwa takwimu na ushahidi wa kutosha . Mheshimiwa Kafulila ni mtu mtulivu , mnyenyekevu na mwenye uwezo wa kujenga hoja kwa data.Ni Tz tu mtu kama Kafulila anaweza kupayuka payuka mambo asiyoyafahamu undani wake na watu wakaamini anajua..ana tabia ya kusoma soma magazeti na taarifa za mitandaoni na kudhani vinampa ujuzi wa kueleza kama anavyosoma..ni vitu vya kukariri tu, hajawahi kufanya analysis yoyote ya kiuchumi au mambo ya fedha inavyotakiwa, kupitia maandiko(makala)..issue ya mikopo kupitia hati fungani huwezi itenganisha na kiwango cha mfumuko wa bei na hata kiwango cha ubadilishaji fedha za kigeni kwa nchi husika dhidi ya nchi nyingine..bei ya hati fungani Kenya au Mauritius haiwezi kufanana au kulingana, na si kweli kwamba ukiona bei ya hati fungani Mauritius iko juu kwa maana ya tarakimu, haimaanishi kwamba bei ya hati fungani Kenya iko chini..tafsiri yake inaweza kuwa bei ya hati fungani Mauritius ni ya chini zaidi ya ile ya Kenya pamoja na kwamba ki-tarakimu inaonekana iko juu zaidi ya ile ya Kenya..ni kwa sababu viwango vya mfumuko wa bei na ubadilishaji fedha za kigeni unatofautiana kati ya nchi hizi mbili.