Kafulila: Serikali kubinafsisha Vivuko vya TEMESA nchini kwa Ubia

Kafulila: Serikali kubinafsisha Vivuko vya TEMESA nchini kwa Ubia

Mzee Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2024
Posts
219
Reaction score
279
Naona Kafulila sasa ameamua
IMG-20240919-WA0168(1).jpg
---
Baada ya kusuasua kiuendeshaji, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imetangaza kubadili mfumo wa utekelezaji wa majukumu yake, kwa kushirikiana na sekta ya umma na binafsi kupitia ubia (PPP).

Kutokana na mabadiliko hayo, Temesa imewaita wawekezaji wa sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuwasilisha mapendekezo ya ushirikiano huo katika huduma za vivuko, karakana za ufundi magari na ufundi umeme.

Kwa mujibu wa taarifa za Temesa, wakala unakuja na mpango huo ikiwa ni miezi mitatu tangu Mwananchi iliripoti mfululizo wa ripoti maalumu zinazoonyesha wakala huo kulemewa na majukumu, kuathiriwa na mifumo na hata kujikuta ikiangukia katika madeni.

Ripoti hiyo iliyotokana na uchunguzi uliofanywa kwa takriban miezi mitatu, ilionesha Temesa kukiuka mpango wa matengenezo ya vivuko na kudaiwa zaidi ya Sh30 bilioni na wasambazaji wa vipuli kwenye karakana zake za ufundi magari.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ndani ya Temesa, wakala huo umewaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya kuwekeza kwenye uendeshaji wa vivuko kupitia mpango wa PPP.

Kamishna wa PPP, David Kafulila akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Septemba 18, 2024 amesema ushirikiano huo unalenga kufanywa katika uendeshaji wa karakana 13 kati ya 30 za wakala huo, sambamba na majukumu mengine kama vivuko na ufundi.

Mwananchi
 
Ni wazo zuri, lakini sio kuuza vivuko vilivyopo
kama mtu binafsi analeta kivuko chake chenye ubora na huduma nzuri hy iko poa
 
Back
Top Bottom