Kafulila: Serikali kubinafsisha Vivuko vya TEMESA nchini kwa Ubia

Naona Kafulila sasa ameamua
---
Baada ya kusuasua kiuendeshaji, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imetangaza kubadili mfumo

Mwananchi
Tatizo hamjui tatizo liko wapi hadi TEMESA kushindwa!
Ni kwamba Serikali hailipi madeni kwa Wakati na hivyo kufanya uendeshaji kuwa mgumu!
Biashara kichaa hiyo ya kwenda kuikopesha Serikali na wewe kubaki unadai mpaka unafilisika.
Ngoja wawekezaji wa kukopesha na kuidai Serikali kwa miaka dahari waje!
 
Hata Serikali yenyewe ikijua Sasa Kuna private hawawezi kukopa
 
Kafulila awe rais wetu
Huyu mwenye Jina alilopewa na Jaji Werema mule Bungeni, ni kama amezidi kwa Kiherehere cha kutetea na kupromote Ubinafsishaji bila kujali kama una manufaa kwetu. Au anapatapo % through back kicks? Imekuwa too much utadhania yeye ndiye mwenye Nafasi ya Pro Kitila au Dr Mwingulu ( the true son of Tanzania).
 
Kutokana na mabadiliko hayo, Temesa imewaita wawekezaji wa sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi🥺🥺🤔🙇🏿‍♂
Utaratibu ukoje ili na sisi wa ndani wadogo tuje kushiriki ? Badala ya kutuletea promo zake humu tu, angekuwa anaweka bayana utaratibu na vigezo husika ili wengi wetu wa ndani tuone kama tunaweza kushiriki. Isije kuwa kama ile DP na Bandari zetu, taarifa kuja kuvuja kumbe Mikataba ilishasainiwa kule kwa Wajomba, na bila haya hata Bunge letu linaletewa kubariki jambo ambalo mchakato wake haukufuata sheria wala taratibu za manunuzi ya umma. Hapo Bunge lilionyesha udhaifu mkubwa sana. Na tunawasubilia huku majimboni waje watuelezee ilikuwaje, hasa wale kama akina King walioenda hata Dubai na kupewa Bakshishi eti ni posho za safari kwenda kuona Ofisi za DP. Ni jina tu lilibadirika ikaitwa posho ya safari but was more than that in nature and size
 
Akipatikana wa kubinafsisha CCM itakuwa poa
Mbona Hiki chama siku nyingi kilishabinafsishwa kwa Wafanya Biashara , na kukitoa mikononi mwa waliokuwa wenye nacho. Sisi wakulima na wafanyakazi ambao tuliporwa Chama Chetu tunahitaji kirudishwe mikononi mwetu kwa wenye nacho. La sivyo hata hizo nembo zetu waziondoe kwenye Bendera yake.
 
Sasa Kivuko mnashindwa kuendesha ni kitu gani wanakiweza kwa ufasaha?
 
Uelekeo wa Kafulila ni mzuri
 
Imekaa njema sana!! Hata Ujenzi wa mwendo kasi uwe na Ubia.

Ujenzi wa barabara uwe na Ubia ,tunakatwa kodi wanapewa TANROAD/EWURA halafu hakuna wanachofanya ,bora Sector binafsi wajenge wakachukue % yao mpaka mkopo wao utakaporudi then wakabidhiwe serikali.

Barabara kibao mbovu hazipitiki ,sector binafsi wazijenge wachukue kodi ,mbona nchi zilizoendelea barabara za kulipia zipo? Unashangaa Dar kuna barabara hazina hata lami halafu ni barabara tu kubwa inasimamiwa na TANROAD.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…