Nafahamu vizuri kabisa anachozungumza Kafulila.
Sikuwa na maana ya kwamba barabara inajengwa na mtu mmoja, la hasha, linaweza kuwa kundi/Kampuni binafsi inayotafuta uwekezaji wa pesa ili ipate faida kwa kukusanya hizo 'toll fees'.
Sisi hapa tunawapa watu/makampuni/Mashirika toka nje kujenga miundo mbinu yetu wazalishe faida, bila kujali sisi tunanufaika kiasi gani (najua kutumia baranbara nzuri ni kunufaika).
Tofauti yetu na huo mfano wa China aliotoa huyo niliyemjibu hapo, China hawakutafutiza wawekezaji toka nje, hata Marekani na barabara zake, hawakutafuta wawekezaji toka nje wawajengee hizo barabara. Serikali imejenga yenyewe, au mashirika ya serikali yamefanya kazi hiyo. Kwa China ni mashirika haya tunayoyaona sasa yametapakaa dunia nzima, ndiyo yaliyohusika na ujenzi wa barabara hizo. Hata kwa Marekani, ni sehemu chache sana zilizojengwa na mashirika binafsi kufanya barabara hizo ziwe biashara.
Sisi hapa, tumejitoa moja kwa moja, tuwape watu toka nje shughuli hiyo. Sisi tunajiondoa! Huu ni ujinga.