Kafulila: Tanzania kwa mara ya kwanza tunajenga barabara za kisiasa za kulipia 150km kutoka Kibaha Pwani-Morogoro bila Fedha ya Serikali

Natamani Sana kuijua kwa undani hiyo mikataba ya ubia wanayotarajia kuingia Watu hawa. Kwa jinsi ninavyofahamu namna wa-Tanzania wengi zaidi walivyo na uelewa Mdogo sana kuhusisha na masuala haya ya UBIA Nina uhakika kwamba Watanzania tunaenda kuingizwa mkenge kwenye Mikataba hiyo. Ni lazima mikataba hiyo itakuwa na sura ya 'mikataba ya ki-Mangungo.'
Anatayarisha mwanasheria wa Serikali ka. A sikosei
 
View attachment 2985383
Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Tanzania Mhe David Kafulila amesema ule mradi wa barabara za kulipia(toll road) uliokwama tangu awamu zilizopita Sasa kwenye awamu hii ya sita umeiva.

Mhe Kafulila amesema, mradi huu utatumia zaidi ya US$ 800 milioni karibu sawa na TZS 2.08Trilioni.

Mhe Mkurugenzi Kafulila amesema barabara zinazokwenda kujengwa zitakuwa ndio barabara Bora zaidi hapa nchi zitakazoishi mpaka miaka 35 bila kufanyiwa Ukarabati mkubwa.

Aidha, Mhe Kafulila amesema nia ni kupunguza msongamano wa magari na watu kati ya Dar-Morogoro-Dodoma ambapo Sasa yule anayehitaji kwenda kwa kasi itamlazimu alipie kiasi Fulani Cha pesa ili apite barabara ya Express.

Mhe Kafulila anaeleza kuwa Tanzania itafunga mkataba na mwekezaji huyo na baada ya mkataba kuisha barabara zitasalia kuwa mali za watoto wa Tanzania.

Kafulila anasema nia kubwa ya Serikali ya Dkt Samia Suluhu ni Watanzania kupata huduma bora kwa gharama nafuu pasina kutumia Fedha ya Serikali.

===​

Jambo zuri
 
Ni ngumu, hii kazi inafanywa na watu wengi sio rahisi kufanya huo uhuni msikilize Vizuri Kafulila
Nafahamu vizuri kabisa anachozungumza Kafulila.
Sikuwa na maana ya kwamba barabara inajengwa na mtu mmoja, la hasha, linaweza kuwa kundi/Kampuni binafsi inayotafuta uwekezaji wa pesa ili ipate faida kwa kukusanya hizo 'toll fees'.

Sisi hapa tunawapa watu/makampuni/Mashirika toka nje kujenga miundo mbinu yetu wazalishe faida, bila kujali sisi tunanufaika kiasi gani (najua kutumia baranbara nzuri ni kunufaika).
Tofauti yetu na huo mfano wa China aliotoa huyo niliyemjibu hapo, China hawakutafutiza wawekezaji toka nje, hata Marekani na barabara zake, hawakutafuta wawekezaji toka nje wawajengee hizo barabara. Serikali imejenga yenyewe, au mashirika ya serikali yamefanya kazi hiyo. Kwa China ni mashirika haya tunayoyaona sasa yametapakaa dunia nzima, ndiyo yaliyohusika na ujenzi wa barabara hizo. Hata kwa Marekani, ni sehemu chache sana zilizojengwa na mashirika binafsi kufanya barabara hizo ziwe biashara.

Sisi hapa, tumejitoa moja kwa moja, tuwape watu toka nje shughuli hiyo. Sisi tunajiondoa! Huu ni ujinga.
 
Mkuu nakuheshimu kwa hoja, ila

Je, kunamtanzania anaweza kuweka 2trl barabarani?
 
Jibu ni HAPANA; na hapo hapo nikufahamishe kuwa hukunielewa. Sijaandika popote kusema kuwa kuna mTanzania wa uwezo huo.
Lakini bila shaka, hata wewe unajuwa kuwa hao wanaotoka nje kuja kujenga barabara za aina hiyo, hawaji na kitita cha namna hiyo toka mifukoni mwao, au syo. Si hili unalijua?
Sasa tunaweza kuanzia hapo na kwenda mbele katika kueleweshana.
 
Hata hivyo hakuna Mtanzania aliyefungwa kutafuta pesa popote ili afanye huo mradi.
 
Lakini ni jukumu la serikali kuwaunga mkono wananchi wake na kuwajengea uwezo wa kufanya mambo ndani ya nchi yao, badala ya kila mara kukimbilia hao wa nje. Kama wewe hulioni hilo, ni wazi kuwa unanufaika na huo mpango wa kutafutiza watakaowanufaisha nyinyi zaidi katika miradi hiyo, mkishirikiana na hao wwatu toka nje.

Wewe hujiulizi sisi wenyewe tutajijengea uwezo lini; baada ya miaka 60 mingine au zaidi? Kwa nini iwe hivyo.
 
Kwakuwa kazi ndio imetangazwa ni wakati wenu ukiwemo wewe mkaomba hiyo kazi.
 
Back
Top Bottom