Kafulila: Tatizo la kukatika umeme limemkimbiza mwekezaji wa kiwanda cha nguo Simiyu

Kafulila: Tatizo la kukatika umeme limemkimbiza mwekezaji wa kiwanda cha nguo Simiyu

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ameeleza bayana kuwa tatizo la kukatika kwa umeme kwa Mkoa wa Simiyu kumesababisha mwekezaji wa Kiwanda cha nguo kinachotumia malighafi ya pamba kushindwa kuwekeza katika Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa alikuwa akitoa maelezo hayo kwa Waziri wa Nishati, Januari Makamba aliyekuwa kwenye ziara Mkoa wa Simiyu

“Ambition ya kuwa na Kiwanda cha Textile imekuwepo kwa muda lakini bado tunakuja pale pale ishu issue ya umeme kwamba tukipata umeme wa uhakika hakuna ambaye atasita kujenga kiwanda cha nguo hapa”

Kafulila na Simiyu threads haziishi humu. Dogo na genge lako fanyeni kazi acheni porojo mitandaoni
 
Kwaiyo Kafulila ajasikia taarifa kuwa Tanesco wanakarabati mitambo ya umeme ambayo ilikuwa haikarabatiwi kwa miaka 5?
Kafulila acha fitina,Mama anafungua nchi na wawekezaji wanakuja kwa wingi,mwambie mwekezaji asubiri mitambo ikarabatiwe fomu yake ya maombi kama Shirika la umeme chini ya uongozi madhubuti wa Maharage Chande tumeiona.😁😁
 
I
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ameeleza bayana kuwa tatizo la kukatika kwa umeme kwa Mkoa wa Simiyu kumesababisha mwekezaji wa Kiwanda cha nguo kinachotumia malighafi ya pamba kushindwa kuwekeza katika Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa alikuwa akitoa maelezo hayo kwa Waziri wa Nishati, Januari Makamba aliyekuwa kwenye ziara Mkoa wa Simiyu

“Ambition ya kuwa na Kiwanda cha Textile imekuwepo kwa muda lakini bado tunakuja pale pale ishu issue ya umeme kwamba tukipata umeme wa uhakika hakuna ambaye atasita kujenga kiwanda cha nguo hapa”

inaweza ikawa sababu mojawapo ya kuliwa kichwa
 
Tuelewe CCM na Serikali yake wanafurahia matatizo na umaskini wa watu wake Kwa maana wanatumia kama Ngazi au fursa ya kujitajirisha.

Kukatika Kwa umeme ni fursa Kwa Makampuni ya marafiki wa waziri wauze mafuta na generators.

Tukatae CCM na kudai KATIBA mpya ilotokana na RASIMU alosimamia Judge WARIOBA kabla haijachakachuliwa.

Ameeeeen.
 
Mataga watakenua sana meno wakiiona hii.
Mkuu 'Yoda', imetokea kuwa kawaida, kila nikiona mada za aina hii inayosikitisha sana, inanilazimu nikukukumbuke wewe.

Lakini naona hapa umeweka robo mstari tu, tena usioeleweka maana yake ni nini hasa!

Kwa maoni yangu kifupi: Hiyo pamba ya Simiyu itapata soko la Rivatex hapo jirani tu kaskazini yetu. Sisi tutaendelea kupiga tuvifua twetu kuwa wazalishaji wakuu wa pamba katika maeneo haya; huku wenzetu wakiteka soko la AGOA na kuwa wauzaji wakuu wa bidhaa hiyo toka Afrika!

Hapa pia inanikumbusha msemo wa waziri mmoja wa zamani wa Biashara, na baadae akawa Sekretari General wa UNCTAD, kwamba sis Tanzania tutakuwa wazalishaji wa mali ghafi, kama hiyo pamba,; wenzetu wa Uganda wao wataichambua na kuiweka sawa tayari kuipeleka viwandani ikatengeneze nguo, huko huko aliko Rivatex, na kuziuza katika soko letu na nchi za nje. Huu ndio mwono aliokuwa akiutabiri waziri huyo, na sasa mstaafu wa UNCTAD, miaka hiyo iliyopita; alivyoona ushirikiano wetu utakavyokuwa katika eneo hili!

Ngoja nikuache na hiki kipande ukipe fikra zako.
 
Tuelewe CCM na Serikali yake wanafurahia matatizo na umaskini wa watu wake Kwa maana wanatumia kama Ngazi au fursa ya kujitajirisha.

Kukatika Kwa umeme ni fursa Kwa Makampuni ya marafiki wa waziri wauze mafuta na generators.

Tukatae CCM na kudai KATIBA mpya ilotokana na RASIMU alosimamia Judge WARIOBA kabla haijachakachuliwa.

Ameeeeen.
Tulidhani habari ya Katiba Mpya ilishaanza, kumbe zilikuwa ndoto!

Sasa sijui ni nani atakaye ongoza waTanzania kuidai na kuipata hii katiba mpya, maanake tuliodhani wapo, kumbe wametekwa!

Ni shiiida sana nchi yetu hii. Hakuna unayeweza kumwamini na kumtegemea kuwa atafanya kweli.
 
Back
Top Bottom