Warioba hajatekwa, Mimi ni huru, wewe je?Tulidhani habari ya Katiba Mpya ilishaanza, kumbe zilikuwa ndoto!
Sasa sijui ni nani atakaye ongoza waTanzania kuidai na kuipata hii katiba mpya, maanake tuliodhani wapo, kumbe wametekwa!
Ni shiiida sana nchi yetu hii. Hakuna unayeweza kumwamini na kumtegemea kuwa atafanya kweli.
Mimi na wewe na Kila MTANZANIA anao wajibu kuidai KATIBA mpya.
Changamoto ni budget imepita bila pesa kutengwa Kwa jambo Hilo.
Tunaendelea kudai Judge Warioba arudishwe Kwa Tume na aape, pesa tunazo wananchi, tutachangia.