Mataga watakenua sana meno wakiiona hii.
Mkuu 'Yoda', imetokea kuwa kawaida, kila nikiona mada za aina hii inayosikitisha sana, inanilazimu nikukukumbuke wewe.
Lakini naona hapa umeweka robo mstari tu, tena usioeleweka maana yake ni nini hasa!
Kwa maoni yangu kifupi: Hiyo pamba ya Simiyu itapata soko la Rivatex hapo jirani tu kaskazini yetu. Sisi tutaendelea kupiga tuvifua twetu kuwa wazalishaji wakuu wa pamba katika maeneo haya; huku wenzetu wakiteka soko la AGOA na kuwa wauzaji wakuu wa bidhaa hiyo toka Afrika!
Hapa pia inanikumbusha msemo wa waziri mmoja wa zamani wa Biashara, na baadae akawa Sekretari General wa UNCTAD, kwamba sis Tanzania tutakuwa wazalishaji wa mali ghafi, kama hiyo pamba,; wenzetu wa Uganda wao wataichambua na kuiweka sawa tayari kuipeleka viwandani ikatengeneze nguo, huko huko aliko Rivatex, na kuziuza katika soko letu na nchi za nje. Huu ndio mwono aliokuwa akiutabiri waziri huyo, na sasa mstaafu wa UNCTAD, miaka hiyo iliyopita; alivyoona ushirikiano wetu utakavyokuwa katika eneo hili!
Ngoja nikuache na hiki kipande ukipe fikra zako.