Warioba hajatekwa, Mimi ni huru, wewe je?Tulidhani habari ya Katiba Mpya ilishaanza, kumbe zilikuwa ndoto!
Sasa sijui ni nani atakaye ongoza waTanzania kuidai na kuipata hii katiba mpya, maanake tuliodhani wapo, kumbe wametekwa!
Ni shiiida sana nchi yetu hii. Hakuna unayeweza kumwamini na kumtegemea kuwa atafanya kweli.
Warioba alishamaliza kazi yake.Warioba hajatekwa, Mimi ni huru, wewe je?
Mimi na wewe na Kila MTANZANIA anao wajibu kuidai KATIBA mpya.
Changamoto ni budget imepita bila pesa kutengwa Kwa jambo Hilo.
Tunaendelea kudai Judge Warioba arudishwe Kwa Tume na aape, pesa tunazo wananchi, tutachangia.
Ndugu, unaamini CDM Ikitokea wakaingia mitini madai ya KATIBA mpya yatafifia?Warioba alishamaliza kazi yake.
WaTanzania, mimi na wewe tunaoitaka hiyo katiba hatuwezi kufanya lolote bila ya usimamizi wa viongozi wanaotambulika kisiasa na taasisi zilizopo.
Viongozi wa kisiasa tuliwategemea CHADEMA watuongoze tujipange kwa umoja wetu ili katiba Mpya ipatikane.
Haieleweki CHADEMA wameyeyukia wapi baada ya "mazungumzo ya maafikiano". Hilo ndilo ninalolisemea hapa kama hukunielewa vizuri uliponi'quote' hapo juu.
Kwani Tanzania iko kwenye list ya nchi zilizoendelea? Ndiyo maana huyo Sukuma gang kapigwa chiniKwa mtu aliyeishi nchi zilizoendelea hawezi hata kwa dakika moja kukubaliana na upumbavu wa kukatika umeme.
Hapana, sidhani hivyo, ila kujiweka pembeni kwa CHADEMA wakati huu kutazidi kuchelewesha matokeo. Itatuchukua muda mrefu kidogo kujipanga upya na kuweka msukumo unaowalazimisha CCM kusalimu amri kwetu.Ndugu, unaamini CDM Ikitokea wakaingia mitini madai ya KATIBA mpya yatafifia?
Ni Kweli CDM wamepoa bt juhudi za ndani ya jukwaa na makundi mengine yanaendeleza jitihada hizo.
Tusichoke, tusikate tamaa.
Ameeen
Mkuu 'Rabbon', nilipojibu hapo juu, mstari huu nilikuwa sijaupa uzito unaostahili kupewa.Changamoto ni budget imepita bila pesa kutengwa Kwa jambo Hilo.
Naamini maridhiano yatasaidia kuwahisha mkwamo. Tutafanikiwa.Hapana, sidhani hivyo, ila kujiweka pembeni kwa CHADEMA wakati huu kutazidi kuchelewesha matokeo. Itatuchukua muda mrefu kidogo kujipanga upya na kuweka msukumo unaowalazimisha CCM kusalimu amri kwetu.
Tutakuwa tumepoteza nyenzo muhimu.
Nimekuwa nikiandika humu, Kwa spidi ya Kobe tunayoenda nayo ktk suala hili, sioni uchaguzi ukifanyika 2025.Mkuu 'Rabbon', nilipojibu hapo juu, mstari huu nilikuwa sijaupa uzito unaostahili kupewa.
Mbona hii inatisha zaidi?
Kwa hiyo sasa kama kuna matumaini ya kuwa na Katiba Mpya, ni hapo 2023/24 ndipo kazi hii itapangiwa fungu?
Muda uko wapi wa kumaliza kazi kabla ya 2025?
Na CHADEMA hili wanalifahamu?
Huenda hapa umepitiwa tu; lakini vipo vyama vingi sana vinavyojiita vya upinzani vilivyo tayari hata leo uchaguzi ukiitishwa.Hakuna chama Cha upinzani kitakachokubali kushiriki uchaguzi huu Kwa KATIBA hii Kwa experience tulioshuhudia 2020.
Kuna TETESI kuwa maridhiano yanayoendelea yanalenga power sharing, kwamba bara wagawane majimbo na upinzani.Huenda hapa umepitiwa tu; lakini vipo vyama vingi sana vinavyojiita vya upinzani vilivyo tayari hata leo uchaguzi ukiitishwa.
ACT wao inatosha kabisa kurekebisha tu sheria inayohusu Tume ya Uchaguzi.
Sijui kama ukimya wa CHADEMA (ukiondoa hayo aliyosema Katibu Mkuu), ni ishara maalum, sijui!
Hili nilishaliongelea siku nyingi zilizopita, hasa baada ya Mbowe kujihusisha solo na Samia katika vikao vyao Ikulu.Kuna TETESI kuwa maridhiano yanayoendelea yanalenga power sharing, kwamba bara wagawane majimbo na upinzani.
Kwamba tuwe kama Zenji, Mfumo huu umefail kule, hatutokubali mambo hayo huku.