Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Mwambieni Kijana.

Hakuna anayekopa huko na kujenga hospitali, uwanja wa mpira, barabara, mashule nk.

Watu wanakopa kustimulate uchumi na kuipeleka hela kwenye uwekezaji wa viwanda, technolojia, makampuni ya mafuta na uchimbaji wa madini na kufadhili oversee projects za uwekezaji na kuboost productions kwenye iconic companies zao kama Boeing, Airbus, Chevron, GMC, DP world, Maerky nk.

Watu hawakopi kuentartain makada na chawa watembee na vibunda, kulipa wanasiasa kupata influence ya kukaa madarakani au kufurahisha wapiga kura ili wakupigie kura.
 
Sasa kujenga Shule au Hospitali sio kustimulate uchumi au haufahamu maana ya kustimulate uchumi?
 
Sasa kujenga Shule au Hospitali sio kustimulate uchumi au haufahamu maana ya kustimulate uchumi?

Hospitali na Shule ni basics ambazo zinaweza kufanywa kwa haraka kupitia investment nyingine zenye return kubwa na ya haraka kupitia uwekezaji kwenye hizi rasirimali zetu.

Ukiisimamia vizuri sekta ya madini, utalii nk, ukacontrol matumizi ya Serikali na kudhibiti wizi , shule na mahospitali unaweza kuyajenga kwa makusanyo hayahaya tu.

Mikopo inahitaji uwekeze kwenye strong investment ambazo zitakupa return haraka na faida kubwa pia mfano uwekezaji kwenye uchimbaji wa gas, chuma, dhahabu, mafuta, makaa ya mawe, bandari, uvuvi, utalii nk
 
Tofautisha mkopo wa Binafsi na Mkopo wa Serikali,

Serikali haifanyi Biashara ila huduma.
 
Tofautisha mkopo wa Binafsi na Mkopo wa Serikali,

Serikali haifanyi Biashara ila huduma.

Serikali sio lazima ikafanye biashara, zipo Iconic projects za nchi ambazo zinakuwa mali ya state lakini operated na private entity.

Serikali inainvest kupitia giants company zake kwa kuweka hisa na mtaji ikiwa pamoja na kuyawezesha makampuni yaliyopo kwenye key projects kama uchimbaji wa chuma, gas, mafuta nk

Nimekupa mfano wa makampuni makubwa ambayo ni icon kwa mataifa kama USA, Russia, UK, Japan, China nk... Unafikiri makampuni kama Chevron, Gazprom, China Hydro, Hyundai Heavy equipment, Airbus, Boeing, Barrick Gold, Anglo Gold nk, unafikiri hizo stable companies ni hela kutoka mifumo ya watu tu, Hapana zipo hela za serikali kama mitaji na faida lazima irudi kwenye mzunguko sio mifukoni Kwa watu lakini pia operation zake ndio zinastimulate uchumi kwa kuleta supply ya mafuta, gas, chuma, usafiri nk hapa wengine hupiga hela pia na mwisho wa siku mzunguko wa hela unakuwa mkubwa sana na Serikali inakusanya kodi nyingi sana.
 
Ukikopa ukawekeza kwenye Hydropower plant ukazalisha umeme, na kuhakikisha watu wote wanatuua umeme Kwa bei ya chini maana yake utalipa mkopo na kustimulate uchumi.

Ukikopa ukaweka mitaji kwenye uchimbaji wa gas ambayo tayari tunayo, ukaenda kwenye negotiation na mtaji maana yake utakuwa na shares nyingi kwenye LNG plant na uchimbaji hapa utalipa deni na kustimulate uchumi.

Ukikopa ukaweka mtaji kwenye uchimbaji wa chuma maana yake utaacha kuimport chuma na baadala yake utakuwa unaexport na bei ya chuma ndani itakuwa ndogo tafsiri yake viwanda vingi production cost itakuwa chini.

Ukikopa ukainvest Kwa small scale miners ukaanza kununua Dhahabu kwao na kureserve bank kuu huku pia ukiweka hisa Kwa giant mining companies zote zinaoperate hapa pamoja na Gold smelter kubwa, unashindwaje kulipa hiyo mikopo na kujenga mashule?
 
Mkuu naona unazunguka hapohapo,

Kila kazi inayotumia pesa inastimulate uchumi,

Nadhani hujaijua vizuri maana ya "ECONOMIC STIMULUS "
 
Anafaa maana tantalila Anaziweza huyu

Ova
 
i
iwe kukopa bila kuiba. Tatizo la Tz ni kuiba kinachoingia
 
Hakuna namna yoyote ya kutengeneza uchumi pasipo kukopa? Yaani lazima tukope ndio mambo yaende sawa?
Namna ipo ila wafanya maamuzi ndo viziwi hawataki kusikia wanaona njia pekee ni mikopo wakati wangeweza kupunguza matumizi yao mfano posho na mishahara ya wanasiasa (bunge) manunuzi ya magari ya kifahali kila mwaka kuziba mianya ya ufisadi kwa kuweka sheria kali kwa atakayebainika kujihusisha na rushwa na matumizi mabqyq ya mali za umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…