Kafulila: UNDP imetoa orodha ya nchi 54 duniani zilizoelemewa na deni la Taifa. 25 zinatoka Afrika Tanzania haipo, tukope zaidi tujenge Uchumi zaidi

Unajua uchumi Wewe?!
Uchumi upi,huo uchumi fake tuliofundishwa vyuoni,tena kwa kutumia waalimu fake waliofundishwa na hao hao waliobuni mikakati ya kutuibia.Mmefungiwa kwenye ma-box ya ujinga,ili waendelee kuwaibia,poleni sana.Mimi simo kwenye ujinga huo,nimeshachomoka.
 
Sasa nyie BAVICHA simsubiri hayo mabaya mnayoiombea Tanzania yatokee

Hakuna anayeombea mabaya yatokee Tanzania Bali ni uongozi mbaya wa CCM . Deni limefika Trilioni 91 kwa uchache. Nani atatusaidia kulipa Hilo Deni?
 
Kafulila hii ni hazina KWELIKWEL

Hazina gani imetbmbuliwa ukuu wa mkoa?. Yule ni chawa tu. Hazina gani inashauri tukope baadala ya kushauri tupunguze madeni na namna ya kupunguza matumizi Kama V8.
 
Jibu hoja. Great thinkers wa JF waliishia wapi? Yaani siku hizi mada hizi Huwa zinaingiliwa na wafia dini wa naniliu. Tabu sana hii

Mtu kushauri kukopa ndio hoja?. Hakuna hoja ya kujibu maana ni kihoja. Kafulila angeshauri tuache kukopa kwa muda na kupunguza Deni lililopo ningemuona wa maana.

Nchi inadaiwa Trilioni 91 halafu kilaza anashauri tukope zaidi, huyo utamjibu Nini?.
 
Credit rating Tanzania iliyopewa na Moody’s ni sawa na F ya 35% darasani, inaonekana afadhali kwa sababu kuna wengine wana F za 20%, 10%, wengine hawana marks kabisa. Lakini in practice F kuanzia 39% wote ni sawa maana lazima warudie mtihani.

Kwa ivyo ukiona hawa jamaa wanajisifia kilichosemwa na Moody’s unajiuliza kama wazima huko vichwani.

Halafu wanataka kujifananisha na nchi zenye credit rating za AAA kama Japan. Akili zetu zinatutosha wenyewe.
 
Acha porojo za kijinga,unaelewa maana ya kujenga njia za Uchumi au unapayuka tuu?

Mipango madhubuti bila nyenzo utakusaidia Nini?

Acha ujinga wewe nzi wa kijani. Kwa hivyo Tanzania bila kukopa haitapata maendeleo. Jifanyeni wajanja wakati akili zenu haziwezi kuleta maendeleo zaidi ya kupambana na CHADEMA.
 
Shida hata hao UNDP sio wa kuaminika. Mfumo wote wa UN usiuamini sana kama wewe ni nchi masikini huku kajamba nani. Mashirika hayo yaliundwa kusaidia mfumo wa kinyonyaji wa nchi tajiri marekani na zile zilitutia kwenye ukoloni. Walitupa uhuru wa bendera tu huku wakihakikisha bado wanatutawala kiuchumi.
Kwa hivyo kama undp kakuonesha hujakopa sana usikurupuke kukopa ovyo.
IMF imeziingiza nchi nyingi matatani kiuchumi kwa masharti yao ya kukopesha. Nchi kama argentina wako hoi ndio maana hata rais na serikali yao hukuwaona kusherehekea kombe la dunia. Nchi iko hoi kiuchumi.
 
Sasa Unataka tumwamini nani?
 
Mtu kushauri kukopa ndio hoja?. Hakuna hoja ya kujibu maana ni kihoja. Kafulila angeshauri tuache kukopa kwa muda na kupunguza Deni lililopo ningemuona wa maana.

Nchi inadaiwa Trilioni 91 halafu kilaza anashauri tukope zaidi, huyo utamjibu Nini?.
Nchi haidaiwi 91 Bali Til.73
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…