Kafulila: UNDP imetoa orodha ya nchi 54 duniani zilizoelemewa na deni la Taifa. 25 zinatoka Afrika Tanzania haipo, tukope zaidi tujenge Uchumi zaidi

Kafulila umekosea sana. Hii ni sawa na kusema "kwakua nimekua natembea na wanawake/me wengi bila kondom na leo nimepima sina HIV basi niendelee kuwa na wapenzi wengi"

Sio sifa kuingia kwenye kundi lililoelemewa madeni, wala sio sifa kukopa sana. Tujenge uchumi unaojitegemea, unaokopa kidogo zaidi, na unaleta manufaa kwa wananchi wake. Lakini pia Value for Money.

Tumekopa over 21trillion kwa kipindi kifupi lakinj mtaani hali ngumu zaidi kuliko.

Kuna kibonzo cha masoud kipanya cha hela zilizoliwa na panya kinatuambia Mengi.

PIa mgogoro wa CCM na Kanisa Katoliki Kigoma nao unatuambia mengi pia
 
Kafulila ni aina ya wasomi kanjanja waliolewa mvinyo wa uongozi. Kundi hili la wanasiasa wanaamini hakuna maisha nje ya siasa.

Wako tayari kusema lolote ili wapate attention na labda wakumbukwe tena na kupewa madaraka ili waendelee kulamba asali. Ni watu wa hovyo sana na hawafai kwa mustakabali wa Taifa.
 
Wewe unafaa kwa lipi mkuu, Huoni hiki alichoandika Kafulila?
 
Umeongea vizuri sana, sasa kafulila njoo hapa utusaidie mi nataka kukopa crdb interest rate is 15-17% per year wakati hao hao japanese wanapata chini ya 5% per year! Pia Wana gracing period ya maana, njoo kwetu huku uulize grace period! Hebu mnapotoa mifano msitoe kwa namna ya uchawa tuu!
Sure kukopa ni kuzuri kama mnaweza lipa, je mlichokopa ndo kile chote kinaenda kinakotakiwa? Je wananchi wa kawaida unawainuaje na unawalindaje ili nao wapate mikopo kuchangamsha uchumi? So forth!
 
Hivi kafulila mbona ulikuwa kijana mzuri sana, ekuaje, so unahamasisha tukope ili tuemeqe na madeni c ndio
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Zacharia Kafulila kupitia ukurasa wake wa Instagram amewafunda wanaolalamika Kuhusu ukuaji wa deni la Taifa huku akisisitiza tukope zaidi ili tujenge uchumi wetu kwani hata Japan ambayo ni nchi ya tatu Duniani kwa Utajiri bajeti yake 40% ni mikopo tuache maneno maneno Tanzania tuko vizuri,
===
Kafulila anasema, Ripoti ya UNDP Nov2022, imetaja nchi54 zenye hali mbaya ya deni la Taifa Dunian, huku 25 zikitoka Afrika wala Tanzania sio miongoni mwao,

Kafulila anaendelea kwa kusema " Ripoti za Taasisi ya MOODY'S, ambayo ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kupima afya ya uchumi kumudu kulipa deni ( MOODY'S, S&P na Fitch zinamiliki 95% ya biashara hii duniani), Agust 2021 na Oktoba 2022 imeonesha Tanzania bado inafanya vema usimamizi wa deni kutokana kupata mikopo ya muda mrefu na nafuu( concessional loans).

Anaendelea kusisitiza, Tukope kujenga uchumi,Ulaya ilikopa kujenga uchumi baada ya vita ya dunia kwa kusaidiwa na USA( Mashal Plan, ) Bajeti ya Japan ya mwaka 2021, nchi ya 3 kwa ukubwa wa uchumi dunaini, asilimia 40% ni mikopo.

Anasema, "Naam, tukope zaidi kujenga zaidi hasa mikopo ya muda mrefu ambayo uwekezaji miradi hii itaongeza msuli wa uchumi wetu kulipa deni.

Mwaka 2021/22 ndio mwaka deni limeongeka kwa trilioni10(BoT- MER) lakn ndio mwaka uchumi uliongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 5.4 kufikia $67.7bn kutoka $62.3bn ambazo ni sawa na nyongeza ya uchumi kwa miaka miwili( 2019/20 na 2020/21),Ndio maana ya kukopa kujenga uchumi.

Marry X-mass & Happy New year
Pambana mwanawane fursa haiji kirahis 🤣🤣🤣🤣
 
Kafulila achana na mawazo ya kukopa kopa ndiyo uonekane baba bora kwa Familia yako!!! Siku zinakuja mdeni wako atataka hela zake wakati uko dhofuli Hali, ndiyo lugha zote utazisahau!!! 😭
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Zacharia Kafulila kupitia ukurasa wake wa Instagram amewafunda wanaolalamika Kuhusu ukuaji wa deni la Taifa huku akisisitiza tukope zaidi ili tujenge uchumi wetu kwani hata Japan ambayo ni nchi ya tatu Duniani kwa Utajiri bajeti yake 40% ni mikopo tuache maneno maneno Tanzania tuko vizuri,
===
Kafulila anasema, Ripoti ya UNDP Nov2022, imetaja nchi54 zenye hali mbaya ya deni la Taifa Dunian, huku 25 zikitoka Afrika wala Tanzania sio miongoni mwao,

Kafulila anaendelea kwa kusema " Ripoti za Taasisi ya MOODY'S, ambayo ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kupima afya ya uchumi kumudu kulipa deni ( MOODY'S, S&P na Fitch zinamiliki 95% ya biashara hii duniani), Agust 2021 na Oktoba 2022 imeonesha Tanzania bado inafanya vema usimamizi wa deni kutokana kupata mikopo ya muda mrefu na nafuu( concessional loans).

Anaendelea kusisitiza, Tukope kujenga uchumi,Ulaya ilikopa kujenga uchumi baada ya vita ya dunia kwa kusaidiwa na USA( Mashal Plan, ) Bajeti ya Japan ya mwaka 2021, nchi ya 3 kwa ukubwa wa uchumi dunaini, asilimia 40% ni mikopo.

Anasema, "Naam, tukope zaidi kujenga zaidi hasa mikopo ya muda mrefu ambayo uwekezaji miradi hii itaongeza msuli wa uchumi wetu kulipa deni.

Mwaka 2021/22 ndio mwaka deni limeongeka kwa trilioni10(BoT- MER) lakn ndio mwaka uchumi uliongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 5.4 kufikia $67.7bn kutoka $62.3bn ambazo ni sawa na nyongeza ya uchumi kwa miaka miwili( 2019/20 na 2020/21),Ndio maana ya kukopa kujenga uchumi.

Marry X-mass & Happy New year
Anahangaikia uteuzi alikuwa hakujiandaa kukaa kijiweni, akajiajiri
 
Back
Top Bottom