Kafulila: UNDP imetoa orodha ya nchi 54 duniani zilizoelemewa na deni la Taifa. 25 zinatoka Afrika Tanzania haipo, tukope zaidi tujenge Uchumi zaidi

Kafulila atakuwa amefulia kweli kweli [emoji23]
Kukopa sio sifa na hasa kama mikopo hiyo inanufaisha ukoo wa panya, mchwa na mafisadi!.

Kwamba hatukuorodheshwa hivyo tukope tu eti deni letu ni stahimilivu? [emoji848]
Mwambie kweli huyo chawa!
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Zacharia Kafulila kupitia ukurasa wake wa Instagram amewafunda wanaolalamika Kuhusu ukuaji wa deni la Taifa huku akisisitiza tukope zaidi ili tujenge uchumi wetu kwani hata Japan ambayo ni nchi ya tatu Duniani kwa Utajiri bajeti yake 40% ni mikopo tuache maneno maneno Tanzania tuko vizuri,
===
Kafulila anasema, Ripoti ya UNDP Nov2022, imetaja nchi54 zenye hali mbaya ya deni la Taifa Dunian, huku 25 zikitoka Afrika wala Tanzania sio miongoni mwao,

Kafulila anaendelea kwa kusema " Ripoti za Taasisi ya MOODY'S, ambayo ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kupima afya ya uchumi kumudu kulipa deni ( MOODY'S, S&P na Fitch zinamiliki 95% ya biashara hii duniani), Agust 2021 na Oktoba 2022 imeonesha Tanzania bado inafanya vema usimamizi wa deni kutokana kupata mikopo ya muda mrefu na nafuu( concessional loans).

Anaendelea kusisitiza, Tukope kujenga uchumi,Ulaya ilikopa kujenga uchumi baada ya vita ya dunia kwa kusaidiwa na USA( Mashal Plan, ) Bajeti ya Japan ya mwaka 2021, nchi ya 3 kwa ukubwa wa uchumi dunaini, asilimia 40% ni mikopo.

Anasema, "Naam, tukope zaidi kujenga zaidi hasa mikopo ya muda mrefu ambayo uwekezaji miradi hii itaongeza msuli wa uchumi wetu kulipa deni.

Mwaka 2021/22 ndio mwaka deni limeongeka kwa trilioni10(BoT- MER) lakn ndio mwaka uchumi uliongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 5.4 kufikia $67.7bn kutoka $62.3bn ambazo ni sawa na nyongeza ya uchumi kwa miaka miwili( 2019/20 na 2020/21),Ndio maana ya kukopa kujenga uchumi.

Marry X-mass & Happy New year
Kafulila hii ni hazina KWELIKWEL
 
Fuatilia mikataba yake ndiyo utajua nchi inauzwa vipi.
Gesi ya mtwara inayotumika ni ile ya wakati wa mkapa inayokuja songas,hakuna gesi nyingine iliyouzwa,ya Lindi inahitaji $30b,michakato inaendelea,huo mkataba unaoujua wewe hebu uweke hapa walau terms zake
 
Usijitoe ufahamu ,bungeni washa discuss sana mkataba wa gesi na ugaigai wake.
 
Sera mbovu za Ujamaa alizoleta Nyerere zinakwamisha uchumi. Hata mikopo iongezeke mara 1000 bado tutabaki nyuma kiuchumi.
 
Huyu atakuwa anaumwa ugonjwa wa akili ama anajitoa ufahamu kwa sababu anazozijua mwenyewe. Kudaiwa ni utumwa sio sifa
Jibu hoja. Great thinkers wa JF waliishia wapi? Yaani siku hizi mada hizi Huwa zinaingiliwa na wafia dini wa naniliu. Tabu sana hii
 
Usijitoe ufahamu ,bungeni washa discuss sana mkataba wa gesi na ugaigai wake.
Sasa si uweke hapa wewe uliyesikiliza bunge na kuelewa kwamba gesi mtwara ishauzwa, tatizo liko wapi!?..au unaimba tu kiitikio Cha gesi imeuzwa kipang'ang'a!?
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Zacharia Kafulila kupitia ukurasa wake wa Instagram amewafunda wanaolalamika Kuhusu ukuaji wa deni la Taifa huku akisisitiza tukope zaidi ili tujenge uchumi wetu kwani hata Japan ambayo ni nchi ya tatu Duniani kwa Utajiri bajeti yake 40% ni mikopo tuache maneno maneno Tanzania tuko vizuri,
===
Kafulila anasema, Ripoti ya UNDP Nov2022, imetaja nchi54 zenye hali mbaya ya deni la Taifa Dunian, huku 25 zikitoka Afrika wala Tanzania sio miongoni mwao,

Kafulila anaendelea kwa kusema " Ripoti za Taasisi ya MOODY'S, ambayo ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kupima afya ya uchumi kumudu kulipa deni ( MOODY'S, S&P na Fitch zinamiliki 95% ya biashara hii duniani), Agust 2021 na Oktoba 2022 imeonesha Tanzania bado inafanya vema usimamizi wa deni kutokana kupata mikopo ya muda mrefu na nafuu( concessional loans).

Anaendelea kusisitiza, Tukope kujenga uchumi,Ulaya ilikopa kujenga uchumi baada ya vita ya dunia kwa kusaidiwa na USA( Mashal Plan, ) Bajeti ya Japan ya mwaka 2021, nchi ya 3 kwa ukubwa wa uchumi dunaini, asilimia 40% ni mikopo.

Anasema, "Naam, tukope zaidi kujenga zaidi hasa mikopo ya muda mrefu ambayo uwekezaji miradi hii itaongeza msuli wa uchumi wetu kulipa deni.

Mwaka 2021/22 ndio mwaka deni limeongeka kwa trilioni10(BoT- MER) lakn ndio mwaka uchumi uliongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 5.4 kufikia $67.7bn kutoka $62.3bn ambazo ni sawa na nyongeza ya uchumi kwa miaka miwili( 2019/20 na 2020/21),Ndio maana ya kukopa kujenga uchumi.

Marry X-mass & Happy New year
Watu wengine mko wajinga sana,mnaona kukopa ni sifa,kukopa sio sifa,sifa ni kujitegemea dah!Kazi kweli kweli.Jamaa wamewalewesha na ujinga,hamuoni wala hamsikii.
 
Back
Top Bottom