Kafungua makanisa na kuweka kipaza sauti katikati ya jamii ni sawa kisheria?

Kafungua makanisa na kuweka kipaza sauti katikati ya jamii ni sawa kisheria?

felakuti

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
659
Reaction score
1,207
Hivi ni watu kukosa akili ama ni nini? Au watu wameshaona fursa kwenye haya makanisa?

Lakini hata kama umeamua kunyaka fursa uwe tajiri kama wachungaji na manabii wengine, ila ndio uje karibu ama katikati ya jamii unaweka hema sjui nini kwenye uwanja labda wa manispaa halafu unaweka na maspika na sauti kubwa, je hili kisheria linaruhusiwa nchi hii?

Halafu usanii mtupu mtu anarukwa na mapepo anapiga makelele wanamuwekea mic mdomoni, kwaio makelele yote ya mapepo ya mchongo tunayasikia, imefikia saivi ukiwa na vipesa kidogo tu unaweza kufanya lolote

Kwa nchi za wenzetu hii unaenda kuripotiwa na unakuja kuchukuliwa na kufunguliwa mashtaka ya kusababisha kero na usumbufu wa watu (Noise pollution).

Sijawahi ona ujinga wa namna hii.
 
Shitholes countries...

Kabisa watu Sasa wanafungua makanisa kwenye makazi ya watu na wanaweka maspika ? Tumefikia huku?

Hii ingekua rwanda, huyo aliefungua angekua lupango...mkuu karibu kwenda kwa mamlaka husika ,, hio sio sawa kabisa
 
Mbona kuna misikiti mingi imefunguliwa kwenye makazi ya watu na wanapiga makelele kwa kutumia maspika yao. Au hujui hilo!?
 
Ubora wake uko wapi hapa ninapoishi kuna msikiti karibu tunaamshwa usiku na mawaidha yao, je na wao wako sahihi?
Mabishano ya dini ipi ni bora huko mimi sipo ila walokole ni kero kubwa .
 
Nawakubali mashahidi wa yehova wanasali kwa kutumia sauti ya Tv, miaka mia hauwezi kujua kama kuna kanisa mpaka uambiwe.

Sijajua kwanini katika mataifa baadhi wamepigwa marufuku.
 
Mabishano ya dini ipi ni bora huko mimi sipo ila walokole ni kero kubwa .
Sipo kwenye ubishani wa dini tatizo lako hoja yako iko biased kwa sababu unayalaumu makanisa ya kilokole juu ya makelele ya muziki wakati na misikiti inafanya hivyo. Hoja yako ingejielekeza juu ya jumba za ibada na sio walokole
 
Upo sawa kabisa ila kwa maoni yangu makanisa ya walokole wanakera mpaka unaweza sema wamewehuka , hayo ni maoni yangu na sio mtazamo mzima wa mada yote🙏
 
Back
Top Bottom