Kagame Cup, Dar es Salaam-Tanzania 2015 Special thread!

Subirin mech zijazo Yanga itakaponunua mechi kwa timu zisizo na uwezo wa kifedha kama ile ya Rwanda .

Kati ya APR na Gor Mahia nani ananunulika kirahisi..?

Kati ya timu hizo ipi ni Klabu yenye fedha....? Kama sio APR.

Kati ya timu hizo, nani amechangiwa fedha ya Team Accommodation kwa ajili ya michuano....?

Unachekesha sana! Aveva amesha waharibu.. Amewaharibia timu yenu ya mchangani hadi sasa mnachanganyikiwa hata mnashangilia timu za wenzenu.

Go goo goo go oooooohhh Yanga Fc.
😂😂😂😂
 

Hayo mashindano sio ligi kuu au kombe la mtani jembe. Hayo ni mashindano ya kimataifa, zaidi ya mpira kuwa burudani pia ni biashara. Asilimia 90% ya wachezaji wa kigeni Tanzania tumewaona kupitia TV za nje then tukawanunua.

Haki ya kuonyesha hayo mashindano kapewa Supersport sababu kwanza anapatikana katika nchi zote washiriki na pia kwa wasio washiriki jumlisha Dunia nzima. Huyo unayetaka kumpigia chapuo mwambie ajitanue asiishie tuu kwenye hizi nchi tatu bali afungue mipaka zaidi na si vibaya kama akianza kupatikana africa nzima. Maybe afakiriwa mashindano yajayo.
 
Tenda ilitangazwa Azam na DSTV waliishondania hiyo Tenda lakini DSTV walishinda, pesa ndefu wakatoa.

DSTV kapata hiyo tenda sababu anapatikana katika nchi zote washiriki. Azam TV mwisho kimbiji hicho ndicho kilichoinyima nafasi hata hivyo kwa mkwanja wote wababe tuu sioni tofauti kubwa
 

Hawa ndo waandishi wanaojotambua...kibongobongo tinaambiwa eti goli limefunhwa na ngoma
 
Haya wale watani wetu wapya wa jadi ndio wanashuka uwanjani leo kumenyana na KCCA. Jana timu ya wananchi kwa mbinde sana na kwakucheza pungufu tumechezea kichapo kutoka kwa Gor Mahia. Tuwaombee wawakilishi wengine wa Tanzania Azam FC a.k.a SHOGA YAKE NA SIMBA. ashinde hii gemu ili mwisho wa mashindano. Mshindi wa tatu awe KMKM, wa pili AZAM na BINGWA YOUNG AFRICAN SPORTS CLUB
 
ndetichia ushalihama chama nini au kukanda maandazi kumekushinda. Njoo mtupie update za chama lenu Azam.

HADI AIBU MIKIA IMEJAA UWANJANI UTAFIKIRI NA WAO WANASHIRIKI
 
Last edited by a moderator:
Sijakuona humu muda sana.Naona ligi kuu ikiisha nawe unapotea

Mkuu nifah nipo sana. Jana nilikuwa madhabahuni, nilipofungua uzi huu nikaona tumefungwa; nikajiuliza kwa nini Yanga huwa tunapoteza kila mechi ya ufunguzi ya mashindano haya? Niliumia sana lakini nikakumbuka kuwa hata mwaka 1993 kule Uganda tulichapwa na SC Villa mechi ya ufunguzi lakini fainali tulichukua kombe mbele ya hao hao SC Villa. Nikakumbuka kuwa mwaka 2012 tulichezea kichapo kutoka kwa Warundi akina Didier Kavumbagu na wenzake tena hapo hapo Dar, fainali tukawafunga Azam, mwisho nikakumbuka pia kuwa msimu uliopita wa VPL mechi ya ufunguzi tulifungwa na Mtibwa Sugar, mwishoni tukatangaza ubingwa hata kabla ya ligi kuisha.

Sijajua ni kwa nini Mungu anaruhusu tufungwe kila mechi ya ufunguzi! Lakini atukuzwe Mungu wetu kwa kutupatia ushindi katika fainali. Inawezekana fainali ya Kagame Cup 2015 ikawa kati ya Yanga na Gor Mahia, ni ombi langu kuwa historia ijirudie kwa kuchukua ubingwa tena, amina.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…