Kagame Cup, Dar es Salaam-Tanzania 2015 Special thread!

Kagame Cup, Dar es Salaam-Tanzania 2015 Special thread!

Kwani bro Danny umesahau na mwaka jana pia na mwaka juzi?
Hebu piga hesabu zako vizuri kisha uniambie Mikia wana miaka mingapi tokea wakose kushiriki kwenye mechi za kimataifa.
Duh kumbe!!!! Aisee hawa jamaa washakuwa WAHAPAHAPA FC
 
Sawa. Mara ya mwisho kashiriki lini?
Usiwe mnafiki.. Jibu unalijua bado unaniuliza mtani!?

Mara ya mwisho walishiriki 2012 hapo Dar na Yanga kunyakua ubingwa wa Kagame Cup. Walikuwa mabingwa wa Tanzania Bara (TZB) mwaka 2011-2012, walipaswa kushiriki 2013 kama wawakilishi wa TZB huku Yanga wakiwa mabingwa watetezi, mashindano yalifanyika Sudan (Darfur) ambapo Serikali ilizuia timu za Tanzania zisishiriki kwa sababu za kiusalama hivyo Mikia hawakushiriki, mwaka 2014 hawakushiriki, 2015 hawashiriki na 2016 hawatashiriki kwa 100% kwa vile hawana sifa.

Mikia FC a.k.a Mchangani FC oyee!
 
Hahahahah Mimi simba dume hujisikia raha sana nikikuita "Mwajuma ndala ndefu"

Simba gani kila mwaka huchukui makombe ya maana wewe unachukua makombe ya pombe tuu (TBL). Nasikia simba sasahivi yuko Lushoto anakula mapeasi
 
Match Day 3: CECAFA KAGAME CUP 2015
Gor Mahia (Kenya ) Vs KMKM (Zanzibar)
Venue; National Stadium, Dar
Time: 4 pm
Telecom ( Djibout ) Vs Khartoum (Sudan)
Venue; National Stadium, Dar.
Time: 2pm
 
Simba gani kila mwaka huchukui makombe ya maana wewe unachukua makombe ya pombe tuu (TBL). Nasikia simba sasahivi yuko Lushoto anakula mapeasi

Mkuu, wana makombe mengi. Walitwaa kombe baada ya kuiadhibu vibaya Majita FC ya Musoma na jingine waliibamiza Ngulyati Stars ya Kahama.
 
Olunga anapiga goli la tatu.Huyu mhandisi mtarajiwa ni hatariii
 
Back
Top Bottom