Kagame Cup, Dar es Salaam-Tanzania 2015 Special thread!

Wa Simba je?

Kama mpira wa Simba Ungelikuwa tayari, nadhani mwaka 2002 usingekuwa mwaka wa mwisho kwenu kuchukua ubingwa wa CECAFA Kagame Cup.

Simba ilicheza leo?
 
Countinho anatumia akili sana...to me was man of the match
 
Mnacheza na Azam lini?

Jumatano saa 10 jioni, ninasikitika kutangaza kuwa siku hiyo ndiyo mwisho wa safari ya Azam katika mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2015 -Dar es Salaam, Tanzania. Tuonane tena miaka ijayo! RIP Azam FC, kamsalimie mikia fc popote pale alipo.

Namshukuru Mungu kwa kunijaalia kuziona siku hizi za huzuni za mikia fc, kukenua kwenu mtasubiri sana hadi Nani Mtani Jembe III mtakapojaribu bahati yenu!

Yanga oyeeee! Simba_ziiiii!.
 
Na iwe kweli. Ni mapema sana kukutana na Azam. Azam inabidi tukutane nae na tumtoe nusu fainali ili akampe salamu wifi yake na shost mwenzie walieshibana Simba
Hahahaaaaa Danny bwana!
 
hivi......hawa Yanga kwa nini wana tabia ya kuwaweka juu mashabiki hivi kwenye kila Kagame cup?

huwa wanaanzaga kwa kufungwa mechi za mwanzo lakini mwisho wanaishia kuchukua kombe. why Yanga why?

trend hii naona inajirudia mwaka huu....mweeee!
 
Kule Nairobi wamekiri kuwa Yanga ni hatari. Masangoma wamejipanga kuhakikisha kuwa Gor Mahia haikutani na Yanga tena.
 
Heri yenu aisee, sisi kila mwaka tunajenga na kubomoa labda mwaka huu tutafanya finishing.
 
Heri yenu aisee, sisi kila mwaka tunajenga na kubomoa labda mwaka huu tutafanya finishing.

Pole sana Mkuu. Msimu ujao lazima mtafanya wonders maana mmesajili vifaa hatari viz. Mwinyi Kazimoto na Mussa Hassan Mgosi.
 
Yanga inazidi kuimarika. Mechi zingine wachezaji Oscar Joshua na Mbuyu Twitte wasiwepo, na Msuva sio wa kumtegemea, ahanzie benchi
 
Heri yenu aisee, sisi kila mwaka tunajenga na kubomoa labda mwaka huu tutafanya finishing.

True Great Thinker. Salute Mkuu Masuke kwa wenye akili watakuwa wamekuelewa kuwa wewe ni mwanamichezo haswa.
 
Last edited by a moderator:
True Great Thinker. Salute Mkuu Masuke kwa wenye akili watakuwa wamekuelewa kuwa wewe ni mwanamichezo haswa.
Viongozi wetu wanatuangusha sana, Singano na Okwi ndo walikuwa roho ya timu msimu uliopita halafu wote wameondoka kwa maana hiyo msimu huu ni kuanza upya tena.
 
Last edited by a moderator:
Msiwazungumzie simba kwan hawako kwenye haya mashindano.hapa ni yanga na azam tu!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…