Marie Antoinette
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 426
- 412
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema hajui kama wanajeshi wa nchi yake wako Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la waasi la M23 na wanajeshi wa Congo yanaendelea.
Sehemu kubwa ya Jumuiya ya Kimataifa inaamini kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23, ambao walidai kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa Congo wiki iliyopita.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takriban wanajeshi wa Rwanda 3,000 hadi 4,000 wanawasaidia wapiganaji wa M23 Mashariki mwa DRC, huku wakiwazidi idadi waasi hao.