Na wote wakiwa huku wanamchukia sana, hata watus wenzake. Wanasema kapitiliza kwa ubaguzi hata ndani ya watusi, anapendelea ukoo wake tu. Ambao wengi walikuwa uganda
kwa kuongezea tu mkuu. Kama mwalimu alivyosema ukianza ubaguzi utaendelea tu. watutsi wana makundi matatu: abanyiginya, abega halafu watutsi wa kawaida (commoners). Hayo makundi mawili ya mwanzo ndio wale watutsi typical kama kina kagame au madam rita, ambao ukiwaona tu urefu na makomwe unawajua mara moja wana damu za kitutsi toka kwa baba au mama, hawa commoners ambao ndio walio wengi kwa hivi sasa mpaka uambiwe kuwa ni watutsi, maana wengi wako kawaida kawaida hawana tofauti na wahutu au hata wabongo for that matter.
Wafalme huwa LAZIMA watoke ukoo wa Abanyiginya, lakini malkia LAZIMA watoke ukoo wa Abega. Kagame anatokea Abega na hata malkia wa mwisho Rwanda ni mama yake mkubwa kagame! Miaka ya 1800 huko malkia mmoja wa Abega alifanya mapinduzi akaweka mtu wa Abega awe mfalme. Tangu hapo koo hizi mbili za Abega na Abanyiginya zikawa na ugomvi mzito wa kugombania madaraka. Hivyo hata ukikusanya watutsi pamoja, wataanza kupangana hapo hapo kulingana na nani abega nani abanyiginya na nani ----- (commoners). Wahutu walivyopindua, waliobaki ambao ndio wengi ni wale commoners ambao hawakuwa na shida sana na wahutu kwani ingawa walipendelewa lakini bado hali zao hazikuwa tofauti sana na wahutu. Ila waliokimbia wengi walikuwa ni hizi koo mbili za wale wafalme, ndio maana hata ukiangalia "waasi" wa DRC utajua tu kina Nkunda, kina ntaganda, kina makenga ni watutsi dizaini gani. hawa walikimbia kutawaliwa na wahutu zaidi kuliko kunyanyaswa kama wanavyodai. Ndio maana majority ya watutsi waliendelea kubaki Rwanda muda wote.
Sasa hicho unachokisema ni kweli kabisa na ubaguzi ulianzia toka uganda huko. Inasemekana hata yule kamanda wa mwanzo wa RPF Fred Rwigema aliuawa kwa ugomvi huu wa abega vs abanyiginya kugombania kuongoza RPF. Hata ugomvi ulitokea pale Museveni alipomsifia Rwigema kuwa yeye ndie alifanya kazi kubwa RPF cheki hapa:
The Observer - Museveni stirs anger in Rwanda.
Na ndio sababu kubwa kwa nini wafalme wa Rwanda hawataki kurudi Rwanda ili hali nao ni watutsi! Imagine hata prince Rwigemera wa ukoo wa mfalme Ndahindurwa alikufa akiwa dereva tax ubelgiji! King kigeli bado yu hai anaishi nyumba za watu maskini marekani, anatumia food stamps (msaada wa chakula)! Wakati huku nyumbani kagame ameuza mali za mfalme na hata yale majumba ya mfalme anayabomoa! eti anaboresha kigali! Hii yote ni kwa sababu ya chuki dhidi ya abanyiginya clan, kwani mfalme akirudi ingawa hatakuwa rais, ile tu kuwapo kutafanya watutsi wamheshimu kuliko kagame ambaye anatokea ukoo wa malkia!je kwa nini koo za wafalme wa Rwanda hawataki kurudi Rwanda, wakati wao ni watutsi au na wao FDLR? Hili swali ukiwauliza hawa "jamaa" humu sijui watajibuje....
so you are very right, vyeo vya Rwanda vinaenda kwa watutsi hawa wa koo hizi mbili, wakati hawa french speakers ambao most of them ni commoners na ndio majority wanatengwa au wanapewa vyeo visivyo na uzito, vyeo vikubwa vyenye maamuzi mazito lazima uwe abega au Abanyiginya. kwa hiyo mtiririko ni: abega/abanyiginya from uganda, abega/abanyiginya from Rwanda, common tutsis, halafu unamalizia na Hutu. Ila kwenye mambo mazito kama jeshi, urais n.k hapo tunarudi tena kwenye Abega vs Abanyiginya.