Inategemea na uwezo wa uelewa wako, utawala ni uongozi, na kuna aina nyingi za uongozi na vigezo pia. Kama ninavyomfahamu Uhuru ama Kagame, ikija kwenye masuala ya demokrasia hawapo, lakini kwa utendaji wanakubalika. Rwanda kainchi kadogo lakini kameinyima Tanzania usingizi kila siku. Kenya kainchi kadogo lakini rais wake ndani ya miaka miwili amefaulu kufanikisha mengi ambayo Tanzania imeshindwa ndani ya zaidi ya miaka kumi.Afrika mambo ya demokrasia tusubiri kwanza, hebu Wabongo muache kupoteza muda mwingi vijiweni mkijadili demokrasia na muanze utendaji.