Kagame: Tupo Tayari kumpiga Tshisekedi

Kenya hapo mbona ndio inaongoza kuuza Madini ya Tanzanite wakati yanapatikana Tanzania tu hapo vipi?
 
Vurugu ya kikundi si sawa na all out war ya taifa na taifa.
DRC ikisema itumie military personnel wake wote na resources zake zote RWANDA haitaweza kupona.
Hiyo Israel unayoisemea unafadhiliwa na USA na UK.
Yenyewe kama yenyewe haina ubavu,na ishaishiwa askari imeanza kulazimisha raia wawe wanajeshi kilazima.
Juzi imetoa waraka Jews Ultra Orthodox nao wajumuishwe katika jeshi kwa kutoa vijana kama 30k,
Orthodox wakaandamana.
Kifupi usifananishe vita ya kikundi cha kiasi na jeshi kwa jeshi.
 
Kenya hapo mbona ndio inaongoza kuuza Madini ya Tanzanite wakati yanapatikana Tanzania tu hapo vipi?
Sijui kama tunajadili huku unaelewa tunachojadiliana..?

Je, hao wakenya wana uhasama, uvamizi wowote kwa tz?
 
Hiki cha mwisho ulichokisema ndio kinachompa kiburi. Kiufupi jamaa amelelewa na amekua katika mazingira ya "Survive for the fittest " na kwasababu mataifa ya ukanda wa Mashariki mwa Africa yamezubaa ndio kete anayoitumia kujiimarisha na kuitengeneza nchi yake. Tusimlaumu kwasababu sisi wengine hatuna viongozi/wanasiasa wenye visions za vizazi vyao vijavyo bali wanaangalia matumbo yao yatajaaje kipindi bado wapo madarakani. Kagame is a dictator for the good future of his country
 
Yaani rwanda iipige dr congo, kagame yuko serious au anatania?
Unakijua unachokisema!?...

Unaijua intelligencia ya Rwanda!?... Rwanda aipige mara ngapi DRC!?....

Na kila siku ni Rwanda huyohuyo anampiga DRC mashariki ya Congo!?

Rwanda ndie anaefanya Congo kila siku iko vitani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…