Kagame: Tupo Tayari kumpiga Tshisekedi

Kagame: Tupo Tayari kumpiga Tshisekedi

Huyu Kagame anaongea nini sasa?
Hivi anadhani kuna mtu hajui kwamba muda wote amekuwa vitani na DRC?

Anadhani kuna mtu hajui kuwa yeye ndio M23?

A 'fight' DRC mara ngapi?
Yule mzee naona anazeeka sasa!
Rwanda inaendesha uchumi wake kwa malighafi kutoka DRC.

PK anaona kabisa mipango yake ya kuijenga Kigari ita_fail baada ya M23 kufurushwa, so anataka vita ili wanaompa msaada wampushi kuiharibu Kinshasa.
 
Kagame Yuko sahihi

Kongo ikubali watusi Walioko Kongo kama raia wao
Mambo ya kuwabagua hawatendei haki
 
Vita siyo ukubwa wa nchi, vita ni intelejensia, kama jeshi la DRC wameshindwa kutokomeza waasi wa M23 ndo wataweza kumpiga Rwanda? Leo Israel yenye eneo kama mkoa wa Kilimanjaro inawajambisha mataifa ya kiarabu makubwa na yenye population kubwa. Vita ni mbinu, ubora wa jeshi na uzalendo, silaha, tumeona jeshi la Rwandan walivyoingia Mozambique waasi walinywea
Israel hana ubavu wa kupigana hata na nchi moja ya kiarabu pasipo msaada wa mashosti zake Marekani na Ulaya.

Kumbuka Israel ipo hapo mashariki ya kati kimkakati ili kulinda maslahi ya wazungu na sio kwamba eti wana nguvu yoyote kijeshi.
 
Jeshi la Kongo dhaifu Sanaa pia halina nidhamuu/utiii.So PK anauwezo wa kuwin battle na target yake akiwin anachimba madini haswaaaa kujinufaisha.
 
Kagame Yuko sahihi

Kongo ikubali watusi Walioko Kongo kama raia wao
Mambo ya kuwabagua hawatendei haki
Na hao watusi wa Congo wakubali kuwajibika kwa serekali ya Congo na si ya Rwanda
 
Museveni kamtoa Obote, rafiki wa Nyerere, huo msaada wa Tanzania kautoa wapi wakati miaka 80 nchi ilikuwa inapumulia machine.
Kagame alikuwa Chief Military Intelligence wa Museveni kuanzia msituni mpaka ndani ya serikali yake .
Nadhani Obote amep
induliwa na Okello, Okello nae ndio alipinduliwa na Museveni.
 
Israel hana ubavu wa kupigana hata na nchi moja ya kiarabu pasipo msaada wa mashosti zake Marekani na Ulaya.

Kumbuka Israel ipo hapo mashariki ya kati kimkakati ili kulinda maslahi ya wazungu na sio kwamba eti wana nguvu yoyote kijeshi.
Viwanda vya Silaha marekani ni vya waisrael
 
Hivi kweli kwa hali mbaya ya Kiuchumi ya Rwanda, kwa Idadi ndogo ya watu inaweza kupigana na DRC?
 
Museveni kamtoa Obote, rafiki wa Nyerere, huo msaada wa Tanzania kautoa wapi wakati miaka 80 nchi ilikuwa inapumulia machine.
Kagame alikuwa Chief Military Intelligence wa Museveni kuanzia msituni mpaka ndani ya serikali yake .
Museven kaishi Kagera,tabora,horohoro wakati wa harakati zake,japo aliwahi ingia lupango tz baada ya kutofautiana na obote,obote hakuja kwenye msiba wa Nyerere, meaning walitofautiana, Nyerere bawa lake liliegemea zaidi kwa museven
 
Back
Top Bottom