Ni kitu kibaya sana kumhukumu mtubkabla hajatenda kosa.
Ni uj8nga kumhukumu mtu mwenye makosa mengi, kwa kuacha makosa aliyoyatenda, na kutumia makosa mnayofikiri atayatenda.
Mimi si mtetezi wa Magufuli. La hasha. Nimemsema sana hapa.
Lakini, katika hili la twrm limits, aneaema hatavunja katiba. Haikuwa lazima aseme hilo, lakini amesema.
Kumzonga kwa hilo, ni kukosa heshima, kukisa adabu, kukisa umakini na kukosa hoja.
Kwa sababu, kila siku Magufuki anafanya makosa. Kwa maneno na matendo.
Amefanya makosa makubwa mengi. Kuanzia kuapisha watu kuwa mawaziri kabla hawajaapishwa ubunge mpaka kukataza m8kutano ya hadhara ya kisiasa inayoruhusiwa na katiba.
Kuanzia kusema atapiga mpaka shangazi za wapinzani mpaka kuingikia biashara ya korosho na kuangusha mapato ya bidhaa za kilimo kwa asilimia 55 ndani ya mwaka mmoja.
Sasa mtu ambaye akifungua mdomo tu inatoka harufu ya ujinga, kwa nini mnamhukumu kwa makosa ambayo atayafanya 2025, wakati kuna makosa mengi kafanya ndani ya miaka minne iliyopita?
Mnawapa msemo wanaosema wapinzani wa Magufuli wanapinga tu, bila hoja.
Ukizushiwa jwamba utaiba mwaka 2025 na kuhukumiwa kwa kisa hilo ambalo hujalifanya bado, utaona hilo ni sawa?
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
Kingine, wapinzani wa Magufuki wanapoongelea kwamba atavunja katiba na kuendelea kuwa rais baada ya term limits kuisha, hilo lina maana kwamba 2020 wameshakubali Magufuli atashinda?
Kama hawamkubali Magufuli, kwa nini wasipigw kampeni aondolewe 2020?
Ukilalamikia uchaguzi wa 2025 wakati wa 2020 hatujafanya, ni kama umekubali tayari Magufuli kashinda 2020.
Sent using
Jamii Forums mobile app