William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Kafara,
Asante kwa changamoto ulizotoa kuthibitisha juu ya moja Utapeli wa Kagasheki na pili ugumu wa yeye kuingia Geneva.
Kama nimekuelewa vema unakubaliana na data aliyotoa FMES juu ya uthibitisho wa ubadhirifu uliothibitishwa na Maodita katika ofisi na haswa katika nafasi aliyokuwa anakalia Kagasheki ndani ya WIPO. Ila unahoji kwa nini basi hakufikishwa mahakamani?
Kwa uelewa wangu na uzoefu nilionao katika mashirika ya kimataifa, fraud kama hii ya Kagasheki ni nyingi mno na kubwa kuliko hata baadhi ya serikali badhirifu za Afrika. Mara nyingi hufanyika kupitia manunuzi na wakati wa operesheni maalumu.Baadhi ya mifano halisi ni ubadhirifu katika ujenzi wa ofisi ya UNHABITAT-Nairobi ambayo kuwekwa kwake wazi kumemghalimu Prof.Tibaijuka kupoteza cheo, ujenzi wa WIPO ofisi-Geneva ambayo Kagasheki anahusika, fraud katika Operesheni Mafuta kwa Chakula iliyofanyika Iraq (Kagasheki anahusika pia). Swali lako hapa ni kwa nini basi hawafikishwi kwenye vyombo vya sheria? Majibu ni mengi na hutegemea saana move ya fraud yenyewe na adhari zitokanazo na fraud hiyo. Ila moja ya sababu ni UN agencies kuogopa kupoteza uaminifu mbele ya wadhamini.Hizi agencies zote zinategemea michango ya wahisani na nchi wanachama kuendesha shughuli zao. Unapochukua mkondo wa sheria unamaanisha kuanika matumizi mabovu ya pesa za wahisani. Si kwamba haitokei kuchukua hatua kwa mkondo wa mahakama,la hasha inatokea ila kwa kuweka maslahi na nini itakuwa picha (image) ya shirika mbele ya wafadhiri. Kwa kuliona hili,mashirika mengi yamechukua chaguo ya KUZIDHATITI badala ya TIBA katika kudhibiti fraud. Mfano bank accounts zote za mfanyakazi wa mashirika haya pamoja na transactions zake zinaangaliwa kwa karibu sana. Kila mwaka anahitajika kuorodhesha mapato yake, mali alizonazo na amezipata vipi. Hii form si kama ile karatasi ya Bunge la Tanzania. Lakini kwa hii kesi ya Kagasheki nijuavyo mie kabla ya mambo kwenda mbali sana alijiondoa WIPO. Maana hata queries za maodita halizijibu akiwa nje ya WIPO akilazimika kusafiri toka Tanzania.
Pili kuhusu ugumu wa yeye kuingia Geneva binafsi sikumaanisha kupata viza bali aibu ya utapeli aliofanya. Nafahamu familia yake bado hipo hapa Geneva na si mtoto wake wala mkewe yuko au alifika kwenye kampeni zake Bukoba. Unajua nyumbani ni nchi ya ajabu sana, mwizi wa fedha nyingi ni shujaa. Unasikia alimanusura Kagasheki angeukwaa Uwaziri wa Mambo ya Nje!
- Ubarikiwe sana mkuu hakuna la kuongeza wala kupunguza!
FMES!